Home Kimataifa Usiku wa tuzo za Manchester United.

Usiku wa tuzo za Manchester United.

8785
0
SHARE

Usiku wa kuamkia leo kulikuwa na tuzo za mchezaji bora wa klabu ya Manchester  United kwa  msimu huu unaoishia wa mwaka 2017,huo ni utaratibu wa vilabu vyote Epl kutoa tuzo kwa wachezaji bora mwisho wa msimu.

Katika tuzo hizo mlinzi wa kulia wa Manchester United Antonio Valencia aliibuka kidedea kama mchezaji bora wa mwaka kutokana na idadi ya kura zilizopigwa na wachezaji wenzake.

Lakini wakati Vanelcia akishinda tuzo hiyo, kiungo Mhisapania wa klabu hiyo Ander Herrera naye alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kutokana na kura za mashabiki,Hererra aliwabwaga Zlatan Ibrahimovich, Paul Pogba na Antonio Valencia.

Tuzo ya goli bora la msimu ilienda kwa Mualmernia Henrikh Mkhtaryan alilofunga kwa mtindo wa scorpion dhidi ya Sunderland na tuzo ya mchezaji bora wa akiba ikienda kwa Axel Tuenzebe ambaye siku za usoni amekuwa akicheza michezo mingi na kikosi cha kwanza.

Tuzo ya mchezaji bora chipukizi ilienda kwa kinda Angel Gomes, Gomes amekuwa gumzo sana katila klabu hiyo na anatajwa kama lulu ijayo ndani ya United, katika tuzo hizo kwa mara ya kwanza kiungo Paul Pogba alionekana pamoja na wenzake tangu kutokea msiba wa baba yake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here