Home Kimataifa “Tulieni, De Gea ni wetu” Mourinho awatuliza mashabiki wa Manchester United.

“Tulieni, De Gea ni wetu” Mourinho awatuliza mashabiki wa Manchester United.

6385
0
SHARE

Habari na tetesi ni nyingi sana katika msimu wa usajili, kila mchezaji anatajwa anakwenda huku na mwingine naye anatajwa kwenda huku nyingine zikiwa habari za kweli na nyingine ni fununu.

Kati ya habari ambayo ameibuka mara mbili mfululizo katika dirisha kubwa la usajili ni usajili wa golikipa wa Manchester United David De Gea ambaye anatajwa kurudi nyumbani Hispania kujiunga na Real Madrid.

Katika majira ya kiangazi mwaka jana habari za De Gea kwenda Real Madrid zilipamba moto na kila mtu akajua muda umefika na De Gea anaondoka, lakini Manchester United walifanikiwa kuzizima tetesi hizo na wamebaki na De Gea.

Msimu huu tena tetesi hizo zimeibuka tena kwa kasi kubwa sana, habari zinadai tayari Real Madrid wamefanya mazungumzo na De Gea huku kitendo cha kuanzia nje katika michezo ya Europa kikitajwa kama dalili za mwisho wa De Gea katika klabu hiyo.

Jose Mourinho amefungua kinywa chake na kusema De Gea ni wao na yuko katika mipango yake ya msimu ujao, na ndio maana tayari ameshamfanya kama kipa namba moja katika mchezo wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi dhidi ya LA Galaxy nchini Marekani.

“David? atakuwepo na atasafiri na sisi kwenda Marekani kujiandaa na msimu ujao wa ligi,ni kipa bora duniani na sisi tunataka kubakiwa na vile vilivyo bora atakuwa mchezaji wetu” alisema Mourinho.

Lakini wakati Mourinho akisema hayo,huenda De Gea asionekane akiidakia tena United kwa msimu huu kwani Mourinho amepanga kumpanga kipa namba tatu katika mechi ya mwisho ya ligi huku ile ya fainali ya Europa akipanga kumchezesha Sergio Romeo.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here