Home Kimataifa Tottenham watoa kipigo cha mbwa mwizi kwa Leicester City

Tottenham watoa kipigo cha mbwa mwizi kwa Leicester City

3225
0
SHARE

Ni kama waliingia wakiwa na hasira za kukosa kombe ambalo limeenda kwa Chelsea, kwani Tottenham waliingia katika uwanja wa nyumbani wa Leicester City na kutoa kipigo mujarabu.

Tottenham wakiongozwa na Harry Kane waliiangamiza Leicester City kipigo cha mabao sita kwa moja huku Kane akiondoka na mpira baada ya kupiga Hattrick na moja la ziada.

Kwa hattrick hiyo inamfanya Harry Kane kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tottenham Hotspur kuwahi kufunga hattrick nne katika msimu mmoja tangia Jimmy Greaves afanye hivyo mwaka 1969.

Mabao hayo manne ya Harry Kane yamempeleka hadi katika kilele cha ufungaji bora msimu huu kwa kufikisha mabao 24 na kumpita Romelu Lukaku aliye na mabao 23.

Magoli mengine ya Tottenham Hotspur yaliwekwa kimiani na Heung Min Son aliyefunga mawili, huku lile la kufutia machozi la Leicester City likiwekwa kimiani na Ben Chilwell.

Lakini matokeo hayo hayabadilishi mbio za ubingwa wa Uingereza kwani tayari bingwa ameshapatikana ila yanawasaidia tu Tottenham kuongeza idadi ya alama ambapo baada ya mchezo huo sasa wanakuwa na alama 83.

Leicester City ambaye anapambana ili angalau aingie kumi bora wanabaki nafasi ya 11 na alama zao 43 na wakiomba Bournamouth afungwe mchezo wao wa mwisho na wao washinde ili kuingia katika kumi bora.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here