Home Kitaifa Mayanga amewajibu wanaohoji kuhusu Ulimwengu kuitwa Stars

Mayanga amewajibu wanaohoji kuhusu Ulimwengu kuitwa Stars

12949
0
SHARE

Kocha wa Stars Salum Mayanga amewatoa hofu wadau wa soka wanaohoji kwamba kwa amemwita Thomas Ulimwengu kwa sababu hajacheza mechi nyingi kwenye klabu yake ya AFC Eskilstuna ya Sweden kutokana na kuwa majeruhi.

Mayanga amesema, kabla ya kumwita Ulimwengu alizungumza nae pamoja na viongozi wa timu yake kama kuna uwezekano wa kumtumia nyota huyo wa zamani wa TP Mazembe na wote walikubali.

“Thomas nilizungumza nae siku tatu nyuma na mara ya mwisho tulizungumza jana lakini pia nilizungumza na viongozi wa timu yake. Juzi alifanyiwa uchunguzi wa mwisho wa afya yake na picha za uchunguzi wa jeraha lake zimeonesha yuko vizuri na tayari alishaanza mazoezi siku 10 nyuma.”

“Aliniambia kwamba yuko tayari kuja kulitumikia taifa na viongozi wa timu yake waliniruhusu kumwita kwa ajili ya mkumtumia.”

Ulimwengu hakuwepo kwenye kikosi cha Stars kilichoitwa mwezi Machi mwaka huu kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki za kimataifa kutokana na mchezaji huyo kusumbuliwa na majeraha.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here