Home Kimataifa Magazeti ya siku ya leo tarehe 19 May.

Magazeti ya siku ya leo tarehe 19 May.

5395
0
SHARE

The Sun.Crystal Palace wanaangalia uwezekano wa kuwanunua Bacary Sagna na Gael Clichy ambao wote mikataba yao inakaribia kikomo Manchester City, kinda wa Kisenegal mwenye miaka 18 Mamadou Coulibaly amepata bahati kutoka katika maisha ya ukimbizi hadi kuichezea Juventus.

The Sun tena linasema Antonio Conte yuko katika mpango wa kumnunua Pierre Aubemayang ili kuziba pengo la Diego Costa endapo ataondoka Chelsea,na mshambuliaji Ashley Barnes wa Burnley anaweza kujiunga na Crystal Palace au Newcastle ambazo zote zimeonesha kumhitaji.

Daily Mail.Claudio Makelele anaweza kupewa nafasi ya kuwepo katika benchi la Swansea baada ya kocha mkuu wa timu hiyo kuamua kuwa na benchi jipya la ufundi, Chelsea na Liverpool zinaweza kumkosa mlinzi wa klabu ya Middlesbrough Ben Gibson baada ya klabu hiyo kusema kuwa hauzwi.

Daily Mirror.Manchester United wanapambana vikali kumnunua golikipa Jan Oblak kutokana na kutokuwa na uhakika wa kubaki na David De Gea, huku Crystal Palace nao wameingia kwenye vita ya kumnunua Jermain Defoe ambae ataondoka Sunderland mwishoni mwa msimu.

Daily Star.Arsenal wako tayari kutuma ofa kwa Juventus ili kumnunua Mario Lemina na Willy Caballero anaweza kuachana na klabu ya Manchester City na kurejea tena katika timu yake ya zamani ya Malaga.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here