Home Kimataifa Yasemavyo magazeti ya Ulaya leo tarehe 18 May.

Yasemavyo magazeti ya Ulaya leo tarehe 18 May.

6504
0
SHARE

The Sun.Klabu ya Everton iko kwenye mpango wa kujaribu kuwanunua Oxlade Chamberlain wa Arsenal na Gylfi Sigurdson wa Swansea ili kuziba nafasi ya Ross Barkley ambaye anaweza kuondoka klabuni hapo, inasemekana klabu ya Chelsea imeshafanya mawasiliano ya awali na mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku ili kumrudisha katika klabu hiyo kwa £70m.

Gazeti la The Sun tena linasema baada ya kutimuliwa na Leicester City msimu uliopita kocha Claudio Ranieri anaweza kurejea katika ligi kuu ya Uingereza lakini safari hii akiifundisha Wataford na klabu za Manchester United na Chelsea wameshindwa na Ac Millan katika mbio za kumnunua Frank Cassie toka Atlanta.

Daily Mail.Baada ya kuboronga akiwa na klabu ya Tottenham sasa kiungo Paulinho yuko njiani kumwaga wino kuitumikia klabu ya Bayern Munich,habari nyingine ni kwamba pamoja na mchezaji wao kuwindwa na timu kubwa lakini Fulham hawana mashaka kuhusu Ryan Sessgon kwani wanaamini atasaini mkataba mpya.

Daily Mirror.Arsene Wenger anapambana sana ili kuweza kumnunua kiungo wa Olympique Lyon Corentin Tollisso, Man City,Man United na Chelsea wanapambana kupata sahihi ya mlinda mlango wa Stoke City Jack Butland ambaye alikuwa majeruhi kwa mwaka mzima.

Daily Star.Klabu ya Tottenham Hotspur inatarajia kufanya uhamisho wa kushtukiza kwa kumnunua mlinzi wa kulia wa Juventus Dani Alves, kocha wa Swansea Paul Clement anafanya mipango ya kumnunua John Terry kutoka katika klabu ya Chelsea na Inter Millan wanatarajia kuanza mazungumzo na Manchester United juu ya usajili wa Ivan Persic ambaye anatakiwa United.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here