Home Kitaifa Serengeti Boys imepata ushindi wa kwanza Gabon

Serengeti Boys imepata ushindi wa kwanza Gabon

8417
0
SHARE

Serengeti Boys imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza kwenye michuano ya AFCON U17 baada ya kuifunga Angola kwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa Kundi B uliochezwa jioni ya leo Alhamini Mei 18, 2017.

Vijana wa Serengeti Boys ndio walikua wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya sita kipindi cha kwanza baada ya Kelvin Naftal kupasia kamba kwa kichwa akiunganisha krosi ya Nickson Kibabage.

Dakika ya 18 Angola walisawazisha bao hilo kupitia kwa Pedro baada ya kutumia vizuri makosa ya safu ya ulinzi ya Serengeti Boys na kufanya timu zote kwenda mapumziko zikiwa sare kwa kufungana 1-1.

Kipindi cha pili Serengeti waliongeza kasi kutafuta bao na kufanikiwa kufunga dakika ya 69 mfungaji akiwa ni Abdul Suleiman baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Yohana Mkomola.

Serengeti Boys imefikisha pointi 4 baada ya kupata pointi moja kwenye mchezo wa kwanza kufuatia kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Mali ambao ndio mabingwa watetezi.

Pointi hizo zinaifanya Serengeti kuwa kwenye mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kwani watahitaji ushindi au sare dhidi ya Niger kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B.

Endapo Serengeti Boys itafuzu kucheza nusu fainali ya AFCON U17 itakua imefuzu pia kucheza fainali za kombe la dunia kwa vijana wa U17 zitakazofanyika nchini India baadae mwaka huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here