Home Kitaifa Furaha ya Kessy kuelekea ubingwa wa VPL

Furaha ya Kessy kuelekea ubingwa wa VPL

11637
0
SHARE

Na Zainabu Rajabu

BEKI wa kulia wa Yanga, Hassan Kessy ameonesha furaha yake kubwa kwa kucheza vilabu vikongwe vya Simba na Yanga nakupata mafanikio hususan kipindi hiki anapoelekea kunyakua ubingwa wa VPL kwa mara ya kwanza akiwa na timu yake ya sasa.

Kessy aliondoka Simba na kuhamia Yanga baada ya kuwa na mgogoro na viongozi wake wa Simba na kuamua kwenda upande wa pili kutafuta mafanikio ya kisoka.

Baada ya game dhidi ya Toto shaffihdauda.co.tz ilimnasa Hassan Kessy ambaye alisema, wakati anaanza kucheza ligi kuu kwa mara ya kwanza hakua akiwaza kuhusu ubingwa.

“Mechi ilikuwa ngumu sana lakini jitihada za mwalimu kutupa wachezaji wake maelekezo ndiyo kilichopelekea kubadilisha matokeo, kwangu mimi ni furaha,” alisema Kessy.

Kessy ambae itakuwa ni mara yake ya kwanza kutwaa ubingwa wa VPL, amewaomba mashabiki wa Yanga wajitokeze kwa wingi kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kushangilia jinsi wanavyopewa ndoo yao.

Kessy ataungana na wenzake waliojiunga na Yanga msimu huu ambao ni Beno Kakolanya, Andrew Vicent ‘Dante’, Emanuel Martin, Justine Zulu katika kusherekea ubingwa wao wa kwanza VPL.

Ligi itafikia tamati wikiendi hii huku mabingwa wa tetesi Yanga wakiwa jijini Mwanza kukipiga dhidi ya Mbao FC huku tukio kubwa likiwa ni timu hiyo kukabidhiwa mwali wao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here