Home Ligi EPL Chelsea hivi mnamsikia Pep Gurdiola?

Chelsea hivi mnamsikia Pep Gurdiola?

6474
0
SHARE

Unakumbuka kile kitabu cha hadithi kuhusu sungura baada ya kushindwa kurukia mkungu wa ndizi aligeuka zake na kuondoka akisema “sizitaki mbichi hizi”

Sasa hadithi hiyo nimeikumbuka baada ya kusikia kauli ya Pep Gurdiola aliyoitoa kabla ya mchezo wao dhidi ya West Brom Albion ambapo City walishinda bao 3 kwa 0.

Gurdiola ambaye tangu anakuja Uingereza kila mtu alijua anakuja kushinda makombe lakini sasa ambapo kombe lishabebwa na Chelsea Gurdiola amesema yeye furaha yake sio makombe.

Gurdiola amesema yeye furaha yake sio kubeba kombe bali furaha yake kubwa ni pale anapokuwa na aina yake ya uchezaji na wachezaji wake wakamsikiliza na kuifuata aina yake ya uchezaji.

“Furaha yangu mimi haitokani na makombe, hayo makombe wakati nachukua tulikuwa tunacheza kwa namna ambayo nilikuwa ninataka na hiyo ndio furaha yangu” alisema Gurdiola.

Hii inamaanisha hadi sasa Gurdiola hana furaha kwani kama timu ikicheza atakavyo ndio inaahinda makombe baasi ina maana hadi sasa City hawajacheza kama Pep anavyotaka.

Gurdiola ambaye ameshauriwa kubadili aina ya uchezaji wake amekataa katakata “kwanini nibadili?hapana mimi ninataka timu yangu icheze vile nitakavyo mimi na ninavyoamini, kama sishindi baasi wenzangu ni bora kuliko sisi”

Katika mchezo wao wa jana Man City waliibuka kidedea kwa mabao ya Yaya Toure, Kelvin De Bruyne na Gabriel Jesus huku la West Brom likifungwa na Robson Kanu.

Arsenal nao ambao jana walicheza huku uwanja wao ukiwa na mashabiki kiduchu mno waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao mawili ya Alexis Sanchez na kuwafanya waendelee kubaki nafasi yao ya 5.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here