Home Kitaifa Niyonzima kuhusu mechi ya Toto

Niyonzima kuhusu mechi ya Toto

11820
0
SHARE

Na Zainabu Rajabu

KIUNGO wa Yanga Haruna Niyozima amekiri mchezo wao dhidi ya Toto Africans ulikuwa mgumu licha ya kushinda bao moja katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Niyonzima ameiambia Shaffidauda.co.tz. kuwa
mchezo ulikuwa siyo rahisi kama watu walivyokuwa wanaona lakini lengo lao ilikuwa ni kupata alama tatu tu.

“Nawashukuru wachezaji wenzangu kwa sababu mchezo huu haukuwa rahisi hata kidogo, lakini tuliweza kuendelea kupandisha mashambulizi kwenye lango la wapinzani wetu na kupelekea kupatika bao moja.”

Mchezaji huyo raia wa Rwanda amesema anawashukuru mashabiki na wapenzi wa Yanga kwa mahaba waliyoyaonesha tangu mwanzo wa ligi mpaka sasa wanapoelekea tamati.

Yanga imefikisha pointi 68 na kurejea kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi na huku ikibakiwa na mchezo moja dhidi ya Mbao FC kabla ya kutangazwa rasmi mabingwa kwa VPL mara tatu mfululizo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here