Home Kimataifa Manchester United Inatamba Kwenye Akaunti Za Fedha Hata Kama Uwanjani Imelala.

Manchester United Inatamba Kwenye Akaunti Za Fedha Hata Kama Uwanjani Imelala.

4145
0
SHARE

Klabu ya Manchester United itakuwa klabu ya kwanza kutoka kwenye ligi kuu ya nchini Uingereza kufanikiwa kuingiza kipato cha paundi Bilioni moja kutokana na zawadi za ushindi na ushiriki katika ligi kuu ya Uingereza ndani ya muda mfupi katika wiki kadhaa zijazo.

Taarifa za utafiti zinasema kuwa mpaka kufikia mwisho wa msimu uliopita zilionyesha kuwa Manchester United ilikuwa imefanikiwa kufikisha kiasi cha paundi milioni 870.3 kuanzia msimu wa mwaka 1992-93.

Vilabu msimu huu vitafikia kuingiza kiasi cha paundi milioni 100 kwa vile vitakavyomaliza kwenye mkia wa msimamo wa ligi hiyo na vitakavyokuwa kileleni vitapata mpaka kufikia kiwango cha paundi milioni 150 na United kwa sasa wapo katika nafasi ya 6.

Taarifa pia zinasema kuwa Arsenal ni timu ya pili katika kukusanya mapato mengi ya ushiriki wa ligi ya kuu ya Uingereza ikiwa na kiasi cha puandi milioni 842.8.

Liverpool na Chelsea wote walikuwa wameingiza kiasi cha paundi milioni 815.wakitofautishwa kwa kiasi cha paundi 56,809 tu katika misimu 24.

Vilabu vyote vinatarajiwa kufikia kiwango cha paundi bilioni moja kutokana na mapato ya ligi lakini Manchester United inaonekana wazi itakuwa klabu ya kwanza kufikia kiwango hicho kabla ya wengine.

Taarifa rasmi zitatolewa na bodi ya ligi mwisho wa msimu huu kwenye majira ya kiangazi juu ya kiasi kamili ambacho vilabu vitalipwa msimu huu.

Ikumbukwe msimu uliopita vilabu vilichukua kiasi cha paundi bilioni 1.64 kwa msimu uliopita 2015-16 na kiwango kinategemewa kuongezeka msimu huu.

VILABU VILIVYOPOKEA FEDHA NYINGI ZAIDI

 1. Manchester United = £870,270,178
 2. Arsenal = £842,767,443
 3. Liverpool = £815,422,132
 4. Chelsea = £815,365,323
 5. Tottenham = £750,281,906
 6. Man City = £723,497,948
 7. Everton = £700,261,154
 8. Newcastle = £649,353,497
 9. Aston Villa = £649,236,912
 10. West Ham = £585,267,008
 11. Sunderland = £544,691,139
 12. West Brom = £469,320,933
 13. Fulham = £469,282,303
 14. Stoke = £440,148,447
 15. Southampton = £413,090,876
 16. Blackburn = £407,374,059
 17. Bolton = £377,782,130
 18. Wigan = £327,522,594
 19. Swansea = £324,027,184
 20. Norwich = £286,386,229
 21. Crystal Palace = £266,351,695
 22. Hull = £257,682,121
 23. Birmingham = £256,856,871
 24. Middlesbrough = £249,050,677
 25. Leicester City = £247,730,615
 26. Portsmouth = £231,278,314
 27. QPR = £206,823,399
 28. Wolves = £197,532,615
 29. Reading = £173,350,044
 30. Burnley = £167,908,143
 31. Charlton = £159,014,046
 32. Watford = £126,834,655
 33. Leeds = £125,476,974
 34. Cardiff = £107,934,984
 35. Derby = £107,637,845
 36. Blackpool = £86,670,041
 37. Bournemouth = £70,843,913
 38. Coventry = £45,864,675
 39. Ipswich = £44,843,315
 40. Sheffield United = £44,775,780
 41. Wimbledon £34,906,015
 42. Sheffield Wednesday = £34,341,926
 43. Bradford = £23,365,274
 44. Nottingham Forest = £20,132,869
 45. Barnsley = £7,673,144
 46. Oldham = £3,418,187
 47. Swindon = £1,895,182
 48. Luton = £1,493,500
 49. Notts County = £1,493,500

JUMLA= £14,788,455,945

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here