Home Kimataifa Yasemavyo magazeti Jumatatu ya leo tarehe 15

Yasemavyo magazeti Jumatatu ya leo tarehe 15

4656
0
SHARE

The Sun. Kiungo wa Manchester United Michael Carrick yuko katika mazungumzo na klabu hiyo ili kuongeza mkataba ndani ya klabu hiyo na pia kuwa kocha wa vijana chini ya miaka 23, gazeti hilo pia linaripoti kwamba wakati Manchester United wanajiandaa kupambana na Ajax katika mchezo wa fainali ya Europa wameingia kwenye mpambano mwingine wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Malmo Pawel Cibicki.

The Sun.Gazeti la The Sun lina habari nyingine kuwahusu Arsenal ambapo taarifa kutoka Ujerumani zinasema wamekamilisha usajili wa mlinzi wa kushoto wa Schalke 04 Sead Kolasinac na kumpa mkataba wa miaka mitano, James Rodriguez ameonekana akionesha ishara ya kwaheri kwa mashabiki wa Real Madrid baada ya mchezo wao dhidi ya Sevilla.

Daily Express.Winga wa Chelsea Willian anafikiria kuendelea kubaki katika klabu hiyo kwa muda mrefu na hivyo kukata tetesi zilizozagaa kwamba anaweza kwenda Manchester United, Andreas Christensen aliyeko Borussia Monchengladbach kwa mkopo akitokea Chelsea anaweza kubaki katika timu hiyo baada ya kuonesha nia ya kumnunua kabisa.

Daily Mirror.Kiungo wa Tottenham Delle Ali ameziweka mkao wa kula klabu za Manchester United na Barcelona ambazo zinamtaka baada ya kusema kwamba “lolote linaweza kutokea”  wakati wa usajili. Mfungaji wa bao lililoipa Chelsea ubingwa Michy Batshuayi yuko mbioni kujiunga na klabu za West Ham, Marseille au Monaco.

Daily Star.Leo gazeti hili limeibuka na habari zinazoihusu Manchester United tu moja inasema klabu hiyo inataka kutumia kiasi cha £110m kuwachukua wachezaji muhimu wa Tottenham akiwemo Eric Dier, Kyle Walker na Danny Rose, lakini pia Manchester United hao hao wamehamisha macho yao kwa golikipa wa Benfica Ederson kuona kama anaweza ziba nafasi ya David De Gea anayetajwa kutimkia Real Madrid.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here