Home Kitaifa Serengeti Boys imeanza AFCON kwa pointi 1

Serengeti Boys imeanza AFCON kwa pointi 1

4495
0
SHARE

Timu ya taifa ya vijana wa Tanzania chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imetoka suluhu (0-0) kwenye mchezo wake wa kwanza wa michuano ya AFCON U17 dhidi ya mabingwa watetezi Mali.

Matokeo hayo hayakuwa rahisi kwa upande wa Serengeti Boys kutokana na kushambuliwa na Mali hususan katika kipindi cha pili cha mchezo lakini waliweza kuhimili vishindo vyao na mwisho wa mechi kutoka na pointi moja.

Serengeti Boys wamepata pointi moja huku wakisubiri michezo yao miwili watakayocheza dhidi ya Angola na Niger ambayo itaamua kama wanasonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo au vinginevyo.

Ikiwa Serengeti Boys itafuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo, watakuwa wamekata tiketi ya kucheza kombe la dunia kwa vijana chini ya miaka 17 mashindano yatakayofanyika India.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here