Home Kimataifa Pep Gurdiola ana siri kubwa kuhusu wachezaji wake

Pep Gurdiola ana siri kubwa kuhusu wachezaji wake

3241
0
SHARE

­­­­­­­ Mambo yamekuwa tofauti na yalivyotarajiwa na wengi toka kocha Pep Gurdiola ajiunge na Man City, wengi tuliamini huenda kwa alivyoanza msimu labda angechukua taji la ligi kuu au taji lolote kubwa msimu huu.

Lakini hadi sasa Gurdiola hawezi kuchukua kombe lolote msimu huu na kwa mara ya kwanza katika misimu 8 mfululizo kama kocha anamaliza ligi akiwa nje ya nafasi mbili za juu ya ligi.

Viwango vya baadhi ya wachezaji vimetajwa kuwa kati ya sababu ambazo zimemfanya Gurdiola kushindwa kufikia malengo yake msimu huu na akidai baadhi yao ni wazuri lakini hawaendani na mfumo wa timu yake.

Tayari mlinzi Pablo Zabaleta ameruhusiwa kuondoka Etihad na iko wazi kwamba msimu ujao Zabaleta hataonekana na uzi wa Manchester City, lakini sio Zabaleta tu bali wapo wengine.

Gurdiola amekiri kwamba kuna wachezaji ambao hawatasaini mkataba mpya na wapo watakaosaini mikataba mipya na hadi sasa anajua orodha ya wachezaji watakaoendelea kukipiga katika klabu hiyo na anajua watakaoondoka.

“Haijalishi kama watacheza katika michezo ya mwisho ya ligi lakini najua tayari tumeshajua nini cha kufanya” alisema Gurdiola, moja kati ya wachezaji wakubwa ambao wanaweza oneshwa mlango wa kutokea Man City ni kiungo wa Ivory Coast Yaya Toure.

Yaya amekuwa hana msimu mzuri sana ndani na nje ya uwanja toka Pep aje na uhakika wa kubaki katika klabu hiyo sio mkubwa, wengine wanaoweza kuondoka ni Jesus Navas, Gael Clichy, Willy Caballero na Bacary Sagna.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here