Home Kimataifa Huku ndiko anaweza kwenda Rodriguez akiondoka Real Madrid.

Huku ndiko anaweza kwenda Rodriguez akiondoka Real Madrid.

19247
0
SHARE

Mwanzo walianza Chelsea, baadae Manchester United nao wakaingia kati lakini sasa Arsenal nao wanatajwa kumtaka mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Colombia James Rodriguez.

Tofauti na Arsenal, klabu za Chelsea na Manchester United wanapewa nafasi kubwa kumnyakua nyota huyo ambaye amekosa nafasi ya kudumu katika kikosi cha Real Madrid.

Chelsea wanaweza kumtumia Eden Hazard ambaye anahitajika Real Madrid kama chambo ya kumnasa mshambuliaji huyo ambaye Antonio Conte anaonekana kumtaka.

Lakini kwa upande wa Manchester United tetesi zimekuwa kubwa mno kwani inasemekana tayari Rodriguez ameshaandaliwa jezi namba 10 katika klabu ya Manchester United.

Kwa sasa jezi ambayo inasemekana Rodriguez anaitaka inavaliwa na Wayne Rooney na hiyo inamaanisha pengine kuna uwezekano Rooney siku zake United zikawa zimefikia mwisho.

Lakini pia shirika moja la utangazaji nchini Colombia limevujisha taarifa kwamba Rodriguez amefanya mazungumzo ya awali na Manchester United na wameshakubaliana katika mazungumzo hayo ya awali.

Hakuna uhakika kwa sasa kwamba Rodriguez ataenda Chelsea au Manchester lakini Arsenal pia wanaweza kuzipiku timu hizo kama walivyozipiku wakati wa usajili wa Mesut Ozil.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here