Home Kimataifa Hazard amewatabiria wachezaji hawa watatu kufanya makubwa kuliko Messi na Ronaldo

Hazard amewatabiria wachezaji hawa watatu kufanya makubwa kuliko Messi na Ronaldo

27497
0
SHARE

Mshambuliaji nyota wa Chelsea Eden Hazard anatajwa kama mchezaji bora nyuma ya Messi, Ronaldo na Griezman kutokana na kiwango bora anachoonesha akiwa na Chelsea.

Lakini Hazard naye ana maoni yake kuhusu ubora wa wachezaji wengine ambapo anaamini kuna wachezaji bora kuliko yeye na ambao wanaweza kuja kukaa juu ya Messi na Ronaldo.

Lakini ni kama Hazard anaona Messi na Ronaldo wameshindikana kwa sasa kwani anaona wachezaji watakaokuwa juu ya Messi na Ronaldo itawabidi wasubirie Messi na Ronaldo wastaafu.

Lakini Eden Hazard ni kama hajaona mchezaji yoyote katika ligi kuu ya EPL ambaye anaweza kukaa juu ya wafalme hao kwaninwachezaji wote aliowataja wanatokea katika ligi zingine.

Hazard katika orodha ya wachezaji watatu ambao anaamini wanaweza kuchukua nafasi ya Messi na Ronaldo amewataja Paulo Dyabala, Antoine Griezman na Neymar kuwa ndio balaa jipya baada ya Messi na Ronaldo.

“Kwa sasa Ronaldo na Messi hakika ni bora, lakini wakisataafu yuko Neymar,Dyabala au Griezman wanaweza kufanya waliyoyafanya au hata makubwa zaidi ya hapo” alisema Hazard.

Eden Hazard pamoja na kukosa tuzo yoyote kubwa katila ligi kuu ya Uingereza lakini anaonekana ndio nguzo kubwa kwa Chelsea kubeba ubingwa msimu huu, kwa sasa Hazard amekuwa akihusishwa na kujiunga na klabu ya Real Madrid.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here