Home Kitaifa Yanga inahitaji pointi 3 kutangaza ubingwa

Yanga inahitaji pointi 3 kutangaza ubingwa

11823
0
SHARE

Yanga wanahitaji pointi tatu pekee ili kutangaza ubingwa wao katika msimu huu kabla ya mechi za mwisho za ligi Mei 20, 2017. Baada ya ushindi wa leo Mei 13, 2017  wa magoli 2-1 dhidi ya Mbeya City, Yanga imefikisha pointi 65 sawa na Simba na inaongoza ligi kutoka na wastani wa magoli ya kufunga na kufungwa.

Kama watapata pointi tatu kwenye mechi yao ya kiporoitakayochezwaJumanne dhidi ya Toto Africans zitaifanya Yanga kutangaza ubingwa katika msimu huu 2016/2017 kwa sababu watafikisha pointi 68 ambapo hata Simba ikishinda mechi yake ya mwisho dhidi ya Mwadui haitasaidia kwa sababu watafikisha pointi 68 sawa na Yanga lakini watahukumiwa na tofauti ya magoli.

Yanga walianza kupata goli la kwanza dakika ya 7 kipindi cha kwanza mfungaji akiwa ni Simon Msuva ambaye aliunganisha kwa kichwa mpira wa krosi ya Hassan Hamisi Ramadhani ‘Kessy’. Mbeya City walisawazisha goli hilo dakika ya 58 kupitia kwa Haruna Shamte baada ya kazi kubwa kufanywa na Ditram Nchimbi kisha kumaliziwa na Shamte.

Obrey Chirwa ameendelea kuonesha ubora wake kwenye ligi ya Bongo baada ya kuifungia Yanga goli muhimu ambalo limeamua mchezo wa leo na kuirejesha timu yake kwenye nafasi ya kwanza ya msimamo wa VPL.

Chirwa amefunga goli hilo akiunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Juma Abdul.

Yanga inaizidi Simba kwa wastani wa magoli 11, Yanga ina wastani wa magoli 43 wakati Simba wao wanawastani wa magoli 32 hadi sasa.

Simba imebakiza mechi moja ili imalize mechi zake zote (30) za ligi kuu Tanzania bara kwa msimu huu, endapo watashinda mechi hiyo watafikisha pointi 68 lakini Yanga wamebakiza mechi mbili (Yanga vs Toto Africans na Mbao FC vs Yanga) wakishinda mechi yao ya dhidi ya Toto watatangazwa rasmi kama mabingwa wapya wa VPL matokeo tofauti na ushindi, yatapelekea bingwa kujulikana siku ya mwisho ya mechi za kufungia ligi.

Ikiwa Simba itafungwa kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mwadui basi Yanga watakuwa mabingwa hata kama watapoteza mechi zao zote mbili za mwisho.

Ushindi wa Yanga kwa leo ni sawa na kulipa kisasi kwa Mbeya City kwa sababu mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa November 2, 2016 Mbeya City walishinda kwa magoli 2-1 mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Matokeo mengine ya mechi zilizochezwa leo

Kagera Sugar 2-1 Mbao FC

JKT Ruvu 0-1 Majimaji

Tanzania Prisons 2-1 Ndanda FC

Mtibwa Sugar 4 -2 Mwadui FC

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here