Home Dauda TV Dauda Tv: Simba imebakiza mechi moja VPL, bingwa bado hajulikani

Dauda Tv: Simba imebakiza mechi moja VPL, bingwa bado hajulikani

10896
0
SHARE

Simba imeandika ushindi wake wa 20 leo Mei 12, 2017 baada ya kuifunga Stand United kwa magoli 2-1 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara. Tayari Simba imecheza mechi 29 na kupata ushindi mara 20, sare tano na imepoteza michezo minne.

Magoli ya Juma Liuzio dakika ya 23 na dakika ya 35 kipindi cha kwanza yanaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 65 na kurudi tena kwenye nafasi ya kwanza ikiiacha Yanga kwa pointi tatu huku wakisubiri mechi ya kesho kati ya Yanga dhidi ya Mbeya City.

Goli la Selemani Selembe dakika ya kwanza ya mchezo ndio lilikuwa la kufutia machozi kwa upande wa Stand United ya Shinyanga.

Stand United imepoteza mechi zote ilizocheza dhidi ya timu za Dar es Salaam (Yanga, Simba, Azam na African Lyon). Yanga iliifunga Stand kwa magoli 4-0, African Lyon ikaifunga 1-0, Azam wakashinda 2-0 na Simba wameifunga Stand 2-1.

Simba ndio timu pekee ya Dar iliyoruhusu kufungwa goli na Stand ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani, timu nyingine zote za Dar zilishinda mechi zao dhidi ya Stand United bila kuruhusu kufungwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here