Home Kitaifa Neno la Mkude kwa wafiwa wa msiba wa Arusha

Neno la Mkude kwa wafiwa wa msiba wa Arusha

7157
0
SHARE

Nahodha wa klabu ya Simba Jonas Mkude ametoa neno la pole kwa wafiwa, ndugu, jamaa na watanzania wote kufuatia msiba wa wanafunzi na walimu wa shule ya msingi St. Lucky Vicent pamoja na dereva msiba uliosababishwa na ajali ya gari wakati wanafunzi hao wakielekea Karatu kwa ajili ya mtihani wa ujirani mwema.4774

Mkude amesema anaungana na watanzania wote kuwapa pole wafiwa walioguswa moja kwa moja na msiba huo uliotokea Mei 6, 2017 mkoani Arusha.

“Kwa upande wa Simba, tumehuzunishwa kwa msiba ambao umetokea napenda kuwapa pole wafiwa kwa niaba ya wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki japo wapo mbali na mimi lakini mwisho wa siku pole yangu ni kitu kizuri sana kwao lakini wakisikia nawapa pole ni faraja pia kwangu, Mungu awape nguvu wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu wanachopitia kwa sasa,” alisema Mkude mara baada ya mechi yao ya ligi dhidi ya African Lyon.

Leo Mei 8, 2017 Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ataongoza wananchi kuwaaga wanafunzi pamoja walimu waliofariki kwenye ajali hiyo shughuli ambayo inatarajiwa kufanyika asubuhi kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here