Home Kimataifa Kwa mara ya kwanza, Wenger amfunga Mourinho katika Epl.

Kwa mara ya kwanza, Wenger amfunga Mourinho katika Epl.

2141
0
SHARE

Kwa mara ya kwanza tangu Jose Moirinho aanze kufundisha soka nchini Uingereza amekubali kufungwa na Arsene Wenger katika ligi kuu ya nchini humo.

Mourinho ambaye hakupanga kikosi kizima anachokiamini, katika mchezo huo aliamua kumpa nafasi kinda Axel Tuenzebe na kuishuhudia United ikifa bao 2 kwa 0.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa na kadi ya njano moja tu, mabao yote yalipatikana katika kipindi cha pili na ndani ya dakika 3 United waliruhusu nyavu zao kuguswa mara 3.

Alianza kiungo wa Arsenal Granit Xhaka katika dakika ya 54 kuzitungua nyavu za United kabla ya dakika 3 baadae mchezaji wa zamani wa Manchester United Danny Welbeck kuiandikia Arsenala bao la pili.

Kwa matokeo hayo Manchester United wanabaki nafasi ya 5 wakiwa na alama 65 lakini huku wamecheza mchezo mmoja zaidi ya Arsenal ambao wako nafasi ya 6 na alama zao 63.

Kabla ya Arsenal na Manchester United kulipigwa pambano kati ya Southampton na Liverpool ambapo mechi hiyo hadi inamalizika hakuna aliyegusa nyavu za mwenzake.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here