Home Kimataifa Nani kama Cristiano Ronaldo?aweka rekodi mpya.

Nani kama Cristiano Ronaldo?aweka rekodi mpya.

24565
0
SHARE

Hakika anastahili kuwa mchezaji bora wa dunia, hakika Ronaldo hana mpinzani kwani kila kukicha yeye anavunja tu rekodi zilizowekwa na wachezaji waliomtangulia.

Katika mchezo wao dhidi ya Valencia ambapo Real Madrid waliibuka na ushindi wa bao mbili kwa moja, Cristiano Ronaldo alifunga bao lake la 20 katika ligi ya Hispania.

Lakini bao hilo la Cristiano Ronaldo limempa rekodi mpya ambayo hapo mwanzo ilikuwa ikishikiliwa na mkongwe wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya England Jimmy Greaves.

Jimmy Greaves hadi anastaafu soka alicheza katika ligi mbali mbali kama Serie A na Epl na katika michezo 528 aliyocheza katika ligi hizo alifunga mabao 366.

Toka kipindi Greaves anastaafu hakuna mchezaji mwingine ambaye ameshawahi kufunga idadi hiyo ya mabao katika ligi kubwa sita barani Ulaya na rekodi hiyo imekaa kwa miaka 46.

Ni Cristiano Ronaldo aliyeweza kuvunja rekodi hii ndefu ya Greaves kwani katika mchezo wake wa 483 Ronaldo alifunga bao lake la 367 katika ligi za ndani za Ulaya.

Ronaldo alifunga mabao 3 katika ligi ya Ureno wakati akiichezea Sporting, akafunga mabao 84 wakati yuko na Manchester United na sasa akiwa Madrid amefunga 279 katika La Liga na kumfanya afikishe jumla ya mabao hayo 367.

Watatu kwa kufunga idadi kubwa ya mabao katika ligi za Ulaya ni mchezaji wa zamani na mkongwe wa timu ya taifa ya Ujerumani Gerd Muller ambaye hadi anastaafu alifunga mabao 365.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here