Home Kitaifa Mzamiru Yassin mchezaji bora March

Mzamiru Yassin mchezaji bora March

6735
0
SHARE

 Zainabu Rajabu.
KIUNGO wa Simba SC Mzamiru Yassin ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa tatu (March) ya timu ya Simba, katika Mwezi wa tatu Simba ilicheza mechi tano ikiwa mechi mbili ni za mashindano ilicheza na Mbeya City kwenye ligi kuu, wakacheza na Madini Fc katika kombe la shirikisho Azam Sports Federation Cup (ASFC) na mechi tatu za kirafiki dhidi ya (Polisi Dodoma,  Chemba Kombaini, na Mererani Kombaini) .

Simba imekuwa na utaratibu mzuri wa kumchagua mchezaji yoyote ambae alionyesha kiwango safi na kuisaidia timu kupata matokeo mazuri na kumtunuku tuzo hiyo kama hamasa kwa wengi kufanya vizuri ili kufanikiwa kuipata tuzo hiyo.

Wachezaji wengine ambao wameshanyakua tuzo hiyo ni Abdi Banda mwezi wa pili, Laudit Mavugo mwezi wa Kwanza. Hii ni Mara ya pili kwa Mzamiru Yassin kushinda tuzo ya Mchezaji bora wa mwezi kwa timu ya Simba.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here