Home Kimataifa Himid Mao hana presha anakula zake tu madafu na baby huku akiisubiri...

Himid Mao hana presha anakula zake tu madafu na baby huku akiisubiri Simba

4744
0
SHARE

Kila kona ya jiji la Dar Es Laam ni homa ya pambano kati ya Simba na Azam, pambano litakalopigwa siku ya Jumamosi jioni pale uwanja wa taifa.

Wachezaji wa pande zote mbili lazima watakuwa katika presha, kwani hata picha zilizozagaa mtandaoni zinawaonesha viongozi wa Simba walipiga kikao na wachezaji wao baada ya mazoezi ya mwisho mwisho.

Lakini hali ni tofauti kwa kiungo mkabaji wa Azam Fc Himid Mao “Ninja”, kwani katika kile kinachoonekana Mao hana presha na Simba alitumia ukurasa wake wa Instagram kupost picha akiwa na mpenzi wake.

Picha ya Mao inamuonesha wakiwa kwenye gari yeye na binti huyo wakionekana wenye tabasamu kubwa na kupiga picha hiyo wakiwa wameshikilia madafu yao mikononi.

Wakati Himid akipost picha hiyo, upande wa pili wenzake Simba walionekana katika picha wamekaa chini mazoezini wakimsikiliza raisi wa klabu hiyo Evans Aveva akizungumza nao.

Aveva anaonekana alikuwa akijaribu kuwasisitiza wachezaji wa Simba juu ya mchezo wao na Azam ambao unaweza kutoa taswira mpya kwa klabu hiyo kuhusu kushiriki michuano ijayo ya kimataifa.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here