Home Ligi EPL Kikosi mchanganyiko cha Man Utd na City cha Shaffih Dauda

Kikosi mchanganyiko cha Man Utd na City cha Shaffih Dauda

11902
0
SHARE

Kuelekea katika mchezo wa Manchester Derby usiku huu kati ya Manchester United na Manchester City katika uwanja wa Etihad, mchambuzi Shaffih Dauda ana kikosi chake.Akifanya mahojiana na mtandao huu Shaffih aliulizwa swali kuhusu kikosi bora kuelekea mchezo huu wa leo na akakitaja huku akimtupa nje Wayne Rooney.

Shaffih kama ilivyo kwa wafuatiliaji wa masuala ya kisoka wengine amemuweka golikipa David De Gea kama golikipa bora wa mchezo huo wa leo.

Kwa upande wa beki wa kulia Shaffih amemtaja mlinzi wa Manchester United Antonio Valencia huku mlinzi wa kushoto akimtaja Aleksandar Kolarov .

Walinzi wa kati Shaffih amemtaja Eric Bailly wa Manchester United huku mlinzi mwingine wa kati akiwa ni kapteni wa klabu ya Manchester City beki Vicent Kompany.
Ander Herrera aliyeko katika kiwango cha juu yupo kama namba sita,huku David Silva akicheza namba saba na Paul Pogba ambaye ni majeruhi akiwa anasimama kama namba nane.

Mshambuliaji hatari wa Manchester City Kun Aguero anasimama kama namba tisa katika kikosi cha Shaffih na Kelvin De Bruyne akisimama kama namba kumi.

Namba kumi na moja katika kikosi hicho ni Henrikh Mkhitaryan, Shaffih amechagua kikosi hicho kutokana na viwango vya wachezaji hao kwa siku za usoni.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here