Home Kimataifa CR7 ana rekodi dhaifu vs Barca @SantiagoBernabeu – leo ataiboresha?

CR7 ana rekodi dhaifu vs Barca @SantiagoBernabeu – leo ataiboresha?

6314
0
SHARE

Real Madrid kwa mara nyingine tena watakuwa wanamtegemea Cristiano Ronaldo kwa ufungaji katika kujaribu kupata ushindi muhimu katika mchezo wa El Clasico usiku wa leo – lakini CR7 ana rekodi dhaifu dhidi ya Barcelona katika uwanja wa Estadio Santiago Bernabeu.

Akiwa ametoka kufunga hat trick katika mchezo vs Bayern, CR7 anaingia katika El Clasico akiwa na nia ya kushinda na kuboresha rekodi yake binafsi dhidi ya Blaugrana katika uwanja wa nyumbani.

Katika mechi 12 za El Clasico jijini Madrid, Ronaldo ameshinda mechi 3 tu, ukilinganisha na 5 katika mechi 13 katika uwanja wa Camp Nou. 

Ronaldo pia amefunga magoli 5 tu vs Barcelona katika uwanja wa Bernabeu wakati akiwa amefunga magoli 10 katika uwanja wa Camp Nou. 

Ni mara tu magoli aliyofunga Ronaldo katika uwanja Bernabeu yalisababisha ushindi kwa Madrid, magoli mengine mawili yaliishia kwenye michezo ya sare na moja likaishia kwenye kipigo.

Usiku wa leo CR7 anategemewa kunza katika Clasico, Je ataweza kuboresha rekodi yake dhidi ya Barcelona katika uwanja wa Santiago Bernabeu? 
Saa 3:45 kupitia Azam TV tutaangalia mtanange huu. 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here