Home Kitaifa Kamati inayojadili kuhusu pointi 3 za Simba imechemsha

Kamati inayojadili kuhusu pointi 3 za Simba imechemsha

32622
0
SHARE

Kikao cha kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji kimemalizika kikao ambacho kilianza tangu asubuhi ya leo April 18, 2017 kwa kujadili mambo mbalimbali lakini suala kubwa ambalo lilikuwa likisubiriwa kusikiwa na wadau wengi wa soka ni suala la Simba kupewa pointi tatu kutoka klabu ya Kagera Sugar kwa madai kwamba klabu hiyo (Kagera Sugar) ilimchezaji mchezaji (Mohamed Fakhi) ambaye alikuwa ana kadi tatu za njano.

Waamuzi wa mchezo kati ya Kagera Sugar dhidi ya African Lyon wote (mchezo unaodaiwa kwamba ndiyo Fakhi alioneshwa kadi ya tatu ya njano mfululizo) waliuwepo pamoja na fourth official, wawakilishi wa Kagera Sugar pamoja na mchezaji Mohamed Fakhi anayelalamikiwa kucheza huku akiwa na kadi tatu za njano lakini pia viongozi wa klabu ya Simba walikuwepo.

Baada ya kikao hicho kumalizika, Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine alizungumza na waandishi wa habari kuwaeleza kilichojiri kwenye kikao hicho ambapo amesema kwamba: “Kamati bado inaendelea kushughulikia suala hilo kwa sababu bado kuna watu muhimu na nyaraka muhimu ambazo inabidi kamati izipitie.”

“Kesho tutawatangazia kikao kinaendelea muda gani na kikao kitakapokuwa kimemaliza shughuli zake, tutawatangazia nini kilichoamuliwa na kikao.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here