Home Kimataifa Ukweli kuhusu tukio la Simba kuanzisha wachezaji 6 wa kigeni dhidi ya...

Ukweli kuhusu tukio la Simba kuanzisha wachezaji 6 wa kigeni dhidi ya Toto.

12994
0
SHARE

Baada ya mchezo kati ya Simba dhidi ya Toto African ya Mwanza kumeibuka taarifa zinazosambaa kwa kasi mitandanoni kuhusu idaidi ya wachezaji wa kigeni walioanzishwa katika mchezo huo na wengi wakisema hilo ni kosa.

Katika mchezo huo Simba walianzisha wachezaji 6 wa kigeni Daniel Aggyei, James Kotei, Bukungu, Laudit Mavugo, Blagnon na Jhuko Murshid na hiyo kupelekea kuibua minong’onk kuhusu idadi ya wachezaji walioanzishwa. Shaffihdauda.co.tz imelifanyia kazi suala hilo na kuona kanuni inasemaje kuhusu hilo.

Kanuni ya 57 ya TFF inayohusu Wachezaji wa Kigeni na jinsi wanavypaswa kutumiwa inatoa utata kuhusu jambo hilo, vifuatavyo ni vipengele 7 vya kanuni hiyo.

(1) Klabu ya Ligi Kuu inaruhusiwa kusajili wachezaji saba (7) wa kigeni kutoka sehemu yoyote duniani na inaweza kuchezesha wachezaji wake wote wa kigeni katika mchezo mmoja wa Ligi Kuu.

(2) Wachezaji wa kigeni watathibitishwa usajili wao baada ya TFF kuhakiki usahihi wa taarifa zao na kukamilika kwa taratibu za uhamisho wa kimataifa.

(3) Mchezaji wa kigeni wa ridhaa anayesajiliwa kwenye Ligi Kuu anaweza kuhamishwa kwa kufuata utaratibu wa uhamisho wa kimataifa kwa wachezaji wa ridhaa.

(4) Wachezaji wa kigeni wanaoruhusiwa kusajiliwa ni wale wanaocheza katika timu za

Taifa za nchi zao au Ligi Kuu ya nchi husika.

(5) Mchezaji yeyote wa kigeni anayesajiliwa katika Ligi Kuu atalipiwa ada maalum ya usajili ya US $2,000 (dola elfu mbili za Marekani) kwa msimu ili usajili wake uweze kuthibitishwa na kuruhusiwa kucheza.

Kanuni hii katika kifungu cha 1 inatoa tafsiri ya wai kabisa kuhusiana na tukio walilofanya Simba katika mchezo huo, hata kama Simba wangeanzisha wachezaji wote 7 bado sheria inaruhusu kufanya hivyo.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here