Home Kitaifa Alichokiandika Mwana FA baada ya Simba kupewa pointi 3

Alichokiandika Mwana FA baada ya Simba kupewa pointi 3

31512
0
SHARE

April 13, 2017 kamati ya saa 72 iliipa Simba pointi tatu na magoli matatu baada ya kujiridhisha kwamba, klabu ya Kagera Sugar ilimtumia mlinzi Mohamed Fakhi kwenye mechi dhidi ya Simba huku mchezaji huyo akiwa ana kadi tatu za njano alizozipata kwenye mechi zilizopita.

Simba ikawasilisha malalamiko yake kwenye kamati hiyo wakidai Fakhi aliitumikia klabu yake kinyume cha kanuni za ligi, baada ya kamati ya saa 72 kujiridhisha na hilo ikaipoka pointi Kagera Sugar na kuipa Simba, pointi hizo zinawafanya ‘Wekundu wa Msimbazi’ kufikisha pointi 61 na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kubeba taji la VPL msimu huu.

Mkali wa Bongofleva Mwana FA kupitia ukurasa wake wa twitter amepost ujumbe akiwakejeli mashabiki wa Yanga wanaolalamika Simba kupewa pointi tatu.

“Tushapewa points 3 zetu…hakuna ubingwa mzuri kama mnaouchukua huku gongowazi wamenuna na wanafoka kama mlevi aliyekoswa na kundi la wezi,” unasomeka ujumbe wa Mwana FA kupitia ukurasa wake wa twitter.

Mwana FA ni miongoni mwa wasaani ambao ni mashabiki wa Simba wasiojificha na mara kadhaa ameonekana uwanjani kuishuhudia klabu yake ikipambana kusaka ushindi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here