Home Kimataifa Stephen Curry Amchapa Lebron James, Warriors Yainyoosha Cavaliers.

Stephen Curry Amchapa Lebron James, Warriors Yainyoosha Cavaliers.

2324
0
SHARE

Mchezaji wa klabu ya Golden State Warriors, Stephen Curry kwa mara nyingine amefanikiwa kuongoza kwa mauzo ya jezi kwa wachezaji wote wanaoshiriki ligi kuu ya mpira wa kikapu nchini Marekani, yaani NBA. Hii inakuwa ni mara ya pili mfululizo kwa mchezaji huyo kufanya hivyo na hii inatokana na takwimu zinazotolewa na mauzo kupitia  NBAStore.com tangu kuanza kwa msimu wa 2016-17 wa NBA.

Kwenye nafasi tano za juu yupo pia mchezaji bora wa kizazi hiki anayechezea klabu ya Cleveland Cavaliers, LeBron James (No. 2), mchezaji mwingine wa Golden State Warriors, Kevin Durant (No. 3), mchezaji anayetegemewa kushinda tuzo ya mchezaji bora mwenye thamani wa NBA (MVP) msimu huu wa klabu ya Oklahoma City Thunder’s Russell Westbrook wakiwa nafasi ya 4 (No. 4) na mchezaji mwingine wa  Cavaliers, Kyrie Irving (No. 5).

Klabu ya Golden State Warriors imeendelea kubaki katika nafasi ya kwanza katika vilabu vinavyouza jezi nyingi zaidi ikifuatiwa na Cleveland Cavaliers, Chicago Bulls wakiwa katika nafasi ya tatu, Los Angeles Lakers namba nne na New York Knicks wakiwa katika nafasi ya 5.

Top 15 ya wachezaji waliouza jezi zaidi:

 1. Stephen Curry, Golden State Warriors
 2. LeBron James, Cleveland Cavaliers
 3. Kevin Durant, Golden State Warriors
 4. Russell Westbrook, Oklahoma City Thunder
 5. Kyrie Irving, Cleveland Cavaliers
 6. Kawhi Leonard, San Antonio Spurs
 7. Kristaps Porzingis, New York Knicks
 8. Jimmy Butler, Chicago Bulls
 9. Giannis Antetokounmpo, Milwaukee Bucks
 10. James Harden, Houston Rockets
 11. Dwyane Wade, Chicago Bulls
 12. Derrick Rose, New York Knicks
 13. Klay Thompson, Golden State Warriors
 14. Isaiah Thomas, Boston Celtics
 15. Damian Lillard, Portland Trail Blazers

Top 10 Ya Chapa Za Vilabu Maarufu Zaidi:

 1. Golden State Warriors
 2. Cleveland Cavaliers
 3. Chicago Bulls
 4. Los Angeles Lakers
 5. New York Knicks
 6. San Antonio Spurs
 7. Oklahoma City Thunder
 8. Boston Celtics
 9. Philadelphia 76ers
 10. Toronto Raptors

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here