Home Kitaifa Maneno ya Manara baada ya Yanga kupinga malalamiko ya Simba kwa mchezaji...

Maneno ya Manara baada ya Yanga kupinga malalamiko ya Simba kwa mchezaji wa Kagera Sugar          

16543
0
SHARE
Haji Sunday Manara, Afisa habari wa Simba SC

Baada ya kamati tendaji ya Yanga kupitia kwa mjumbe wake Salum Mkemi kutanganza kupinga malalamiko ya Simba dhidi ya Kagera Sugar kwa kumtumia mchezaji wao Mohamed Fakih kwenye mechi kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba, afisa habari wa Simba Haji Manara ameibuka na kutoa taarifa rasmi akiwataka Yanga kutulia.

Kwa upande wao Yanga wanasema, Fakih amekubali kwamba ana kadi tatu za njano lakini kadi hizo sio zote alipata kwenye mechi za ligi kuu. Kadi mbili alioneshwa kwenye michezo ya ligi kuu lakini kadi moja alioneshwa kwenye mchezo wa FA Cup.

Manara amewaambia Yanga waache kuishinikiza Bodi ya Ligi itoe maamuzi wanayotaka wao badala yake waiache ifanye kazi yake.

“Nimesikitishwa na taarifa iliyotolewa na viongozi wa Yanga  Salum Mkemi akiwemo mtu anayeheshika sana kwenye mpira wa Tanzania Charles Boniface Mkwasa, nimesikitika sana kumuona kaka yangu Mkwasa.”

“Kazi ya kamati ya masaa 72 hata sisi tulitegemea wangetoa taarifa juzi, lakini wakata kujiridhisha na ni haki yao ili wafanye maamuzi yaliyosahihi. Wakasema siku ya Alhamisi wata watatoa taarifa ya uamuzi waliochukua, sasa Yanga kutoa tamko la kuishinikiza bodi ya ligi kufanya maamuzi wanayotaka wao si sahihi kwa sababu sio ajabu Simba kukata rufaa, hata Yanga wamekata rufaa dhidi ya African Lyon.”

“Sio mara ya kwanza kwa Simba kukata rufaa, tulishawahi kupoteza pointi tatu dhidi ya Kagera Suga miaka ya nyuma, kinachotakiwa ni je, tunao ushahidi wa kuthibitisha rufaa yetu? Hiyo ni kazi ya Bodi ya Ligi, Yanga kazi yao ni kucheza mpira halafu wanayo mambo mengi ya kushughulika nayo, wanatatizo la kutolipa mishahara wachezaji, kiwanja chao cha Kaunda kimegeuga bwawa la kufugia kambale kwa nini waishughulike na yao wanahangaika na ya Simba?”

“Kwani Simba haijawahi kunyang’anywa pointi? Kwa nini iwe ajabu kwa Simba kudai haki, lakini Simba ikidaiwa haki ni sawa tumeshakatiwa rufaa mara ngapi? Tumeshapoteza haki mara ngapi Bodi ya Ligi na TFF?”

“Leo hii wanashikilia habari ya Banda, hakuna kiongozi anayekubali kwamba alichokifanya Banda ni sahihi, mimi mwenye nimemkabili Bnda nikamwambia hapana umekosea, mchezo wa kupigana uwanjani haufai tena nilimwambia tangu alivyofanya hivyo kwenye mechi yetu dhidi ya Yanga. Lakini Yanga kama uongozi mbona hawakusema wakati Ngoma alipompiga Kessy? Fufaa yetu ina miaka miwili pale TFF tangu Kessy anacheza Yanga, mbona hawakusema wachezaji wao walipomtoa kwa machela mchezji wa African Sports? Ila inapokuja kwa Simba kudai haki zao presha inakuwa kubwa tunabebwa.”

“Mchezaji akicheza na kadi tatu tusiseme kisa tunaogopa kuambiwa tunabebwa, tunazitaka hizi pointi. Wao walipata ushindi wa uwanjani tunakubali, lakini wakamchezesha mchezaji kinyume cha taratibu , tunazihitaji hizi pointi na zitatufaa na ni zetu na ni haki yetu na tutazipata.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here