Home Kimataifa Hivi ndio vipigo vikubwa kwa timu 10 za juu Epl.

Hivi ndio vipigo vikubwa kwa timu 10 za juu Epl.

8542
0
SHARE

1.Chelsea. Kipigo chao kikubwa msimu huu walikipokea toka kwa Arsenal wakapigwa bao 3 kwa 0. Ilikuwa kipindi ambacho Conte anaanza EPL na alijaribu mfumo wa kawaida wa Chelsea akachezea goli hizo lakini alipoiweka 3-4-3 yake mchezo ulitulia.

2.Tottenham. Hostspur ambao ndio vinara wa kutoa dozi kubwa kwa timu zingine, nao walikutana na kipigo kutoka kwa Liverpool, kufungwa magoli 2 kwa 0 ilikuwa ndio kipigo kikubwa kwao.

3.Manchester City, City wao msimu huu watu ambao waliwaadhiri walikuwa Everton tena wakiongozwa na makinda Lookman na Tom Davies, mchezo huu ulibadilisha upepo wa City katika mbio za ubingwa, walipigwa 4 kwa 0.

4.Liverpool. Liverpool walikutana na dhahma walipoifuata Leicester City, kwani kipigo cha 3 kwa 1 kiliwazima vijana wa Klopp.

5.Manchester United. Kipigo ambacho kilionekana kumuwewesesha Jose Mourinho na mashabiki wa United ilikuwa 4 bila toka kwa Cheslea, United wanawasubiri Chelsea wiki ijayo kujaribu kulipiza.

6.Arsenal. Kipigo cha juzi toka kwa Crystal Palace cha bao 3 kwa 0 ni kikubwa kwao na pia cha aibu. Mchezo huu umezidisha presha kwa Wenger kwani wameanza kupoteza muelekeo wa kupanda juu.

7.Everton. Everton ambao msimu huu wanaonekana hatari sana, walitepeta mbele ya Chelse baada kufungwa mabao 5 kwa 0 pale Stamford Bridge.

8.Southampton. Southampton wakiwa uwanjani kwao St Marrys waliwakaribisha Tottenham waliokuwa wa moto, kilichofuatia hapo ni Southampton kupokea kipigo cha bao 4 kwa 1.

9.West Bromich. Kocha wao alidai hela za City na uwekezaji wao ndiyo viliwaua,wakiwa nyumbani waliikaribisha Man City lakini walifungwa mabao 4 kwa 0 hapohapo nyumbani kwao.

10.Watford.Pengine hiki ni kipigo kikubwa zaidi, Watford walisafiri kuifuata Liverpool Anfield, Liverpool waliwashambulia sana Watford na kuwafunga goli 6 kwa 1.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here