Home Kitaifa Chirwa hayupo kwenye orodha ya wachezaji wa Yanga watakaosafiri kwenda Algeria

Chirwa hayupo kwenye orodha ya wachezaji wa Yanga watakaosafiri kwenda Algeria

11279
0
SHARE

Klabu ya soka ya Yanga SC inapenda kutoa taarifa juu ya safari yake hapo kesho kuelekea Algeria katika mechi ya marudiano dhidi ya Mc Alger.

Msafara wa wachezaji 20, benchi la ufundi na viongozi utaondoka kesho jioni majira ya saa 12 kwa ndege ya shirika la Emirate kupitia Dubai.

Wachezaji watakaondoka ni Makipa: Deogratius Munishi na Beno Kakolanya.

Nafasi ya ulinzi: Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vicent Bossou , Juma Abdul , Vicent Andrew, Oscar Joshua, Mwinyi Haji, Hassan Kessy na Kelvin Yondani.

Viungo: Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deusi Kaseke, Said Makapu, Juma Mahadhi, Simon Msuva, Geoffrey Mwashiuya na Emmanuel Martin.

Upande wa washambuliaji ni Amissi Tambwe na Donald Ngoma.

Wachezaji wafuatao wataukosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali Justine Zulu, Malimi Busungu, Matheo Antony, Ally Mustapha, Pato Ngonyani, Obrey Chirwa na Yusuph Mhilu.

Imetolewa na idara ya habari na mawasiliano
Young Africans SC
12/04/2017.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here