Home Kimataifa Coutinho aweka rekodi mpya EPL.

Coutinho aweka rekodi mpya EPL.

5385
0
SHARE

Stoke City wakiwa uwanjani kwao walimaliza kipindi cha kwanza wakiwa wanakngoza goli moja dhidi ya Liverpool, lakini sub ya Firminho na Coutinho ilibadilisha hali ya hewa baada ya Coutinho kuwasawazishia Liverpool kabla ya Firminho kufunga bao la pili na mchezo kuifanya Liverpool kumaliza mchezo huo kwa ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.

Kabla ya mchezo huo Mbrazil mwingine Juninho ambaye anachezea klabu ya Middlesbrough alikuwa ameshafunga magoli 29 na alikuwa ndio Mbrazil anayeongoza kwa ufungaji wa magoli katika ligi ya Uingereza huku wakiwa sawa na kiungo huyo wa Liverpool Phillipe Coutinho ambaye naye alikuwa na magoli 29.

Lakini goli la jana la Coutinho dhidi ya Stoke City limemfanya Coutinho kufikisha magoli 30 ambayo yanamfanya kuwa Mbrazil kinara wa magoli katika ligi ya Uingereza, magoli hayo 30 Coutinho ameyafunga katika michezo 132,akifuatiwa na Juninho ambaye ana magoli 29 katika michezo 125.

Kiungo wa zamani wa Chelsea Oscar ambaye sasa amacheza soka nchini China katika michezo 131 aliyoichezea Chelsea amefunga magoli 21 akiwa nafasi ya nne. Roberto Firminho amecheza michezo 60 tu katika ligi ya Uingereza lakini yuko nafasi ya 4 akiwa amefunga jumla ya magoli 20.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here