Home Kitaifa Majibu ya Mbaraka Yusuph ndani ya Sports Extra yamewashangaza wengi

Majibu ya Mbaraka Yusuph ndani ya Sports Extra yamewashangaza wengi

29221
0
SHARE

Kipindi cha Sports Extra kilichoruka April 5, 2017, kilifanya mahojiano na Mbaraka Yusuph mshambuliaji wa Kagera Sugar na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ambaye pia ni mchezaji bora wa mwezi March lengo la mahojiano hayo ikiwa ni kutaka kufahamu mambo kadhaa kuhusu nyota huyo anayefanya vizuri kwa sasa hapa Bongo.

Kitu ambacho kimewashtua wengi na kuwangaza ni pale Mbaraka aliposema kwamba, hafatilii mechi za Ulaya wala hakuna timu yoyote ya ng’ambo anayoishabikia na hadhani kama anaweza kujifunza kitu kutoka kwa mastaa wa wanaotamba kwenye soka la Ulaya.

“Kwakweli wachezaji wa kibongo sio kama tunaweza kujifunza kutoka kwa wachezaji wa Ulaya kwa sababu wao ni ma-profesional zaidi kuliko sisi, labda tuangalie timu nyingine za karibu yetu ambazo si za Tanzania.”

Sports Extra: Ni timu gani unayoishabikia barani Ulaya?

Mbaraka Yusuph: Hakuna timu yoyote nayoishabikia barani Ulaya, pia hata kufatilia mechi za nje huwa ni mara chache, hata nikiangalia mechi basi huwa naagalia kipindi kimoja inatosha.

Sports Extra: Kuna chezaji yeyote anayekuvutia kutokana na uchezaji wake kutoka Ulaya?

Mbaraka Yusuph: Mchezaji ambaye mimi nampenda ni Ronaldinho ‘Gaucho’ ni mchezaji ambaye amekamilika kwa kila kitu.

Sports Extra: Ukiwa nyumbani huwa unapenda kufanya nini?

Mbaraka Yusuph: Maisha yangu ya nje yapo tu kawaida, huwa napendelea kupumzika (kukaa nyumbani) na kuangalia movies.

Sports Extra: Usingekuwa mchezaji, unadhani ungefanya kazi gani?

Mbaraka Yusuph: Ningekuwa mfanya bishara wa kawaida, naona bishara ambayo mtu unaweza ukakaa na kutulia sio kama biashara nyingine.

Baada ya kufanikiwa kutwa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu Tanzania bara kwa mwezi March, mshambuliaji Mbaraka Yusuph amesema kwamba alistahili kupata tuzo hiyo na akaweka wazi kwamba tayari kuna timu ambazo zinahitaji huduma yake japo hakua tayari kuziweka hadharani.

“Najisikia faraja kushinda tuzo hiyo lakini naichukulia kama changamoto ya kuendelea kupambana na namshukuru Mungu kaweza kunijalia nimepata tuzo ambayo inawaniwa na wakongwe wengi.”

“Nastahili kuichukua hii tuzo kwa sababu nimeisaidia sana timu yangu. Mipango yangu ya badae nataka kwenda kucheza mbele zaidi kama Mungu akinijaalia.”

Sports Extra: Kutokana na mafanikio uliyonayo hadi sasa, kuna timu zozote ambazo zimeonesha nia ya kuhitaji huduma yako?

Mbaraka Yusuph: Zipo timu ambazo zinanihitaji hapahapa ndani ila siwezi kutaja ni timu gani kwa sasa, ningependa kwenda kwenye timu ambayo natamani kwenda ni ile ambayo watakuwa wanatekeleza kile ambacho nakihitaji.

Mbaraka anaungana na wachezaji wengine kama Benoit Assou-Ekotto, Bobby Zamora, Dani Alves, Sylvain Distin Stephen Ireland na wengine kibao ambao mchezo wa soka sio kitu wanachokipenda kwa asilimia 100 licha ya wao kuwa wachezaji wenye majina makubwa duniani.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here