Home Kimataifa Baada ya kusemwa vibaya, Shaw amjibu Mourinho.

Baada ya kusemwa vibaya, Shaw amjibu Mourinho.

16718
0
SHARE

Habari kubwa wiki hii katika klabu ya Manchester Unite ni kuhusu Jose Mourinho kumsema Luke Shaw, Mourinho alidai Shaw ana utoto sana na hivyo inambidi ajitambue.

Hii sio mara ya kwanza kwa Josee kumshambulia Shaw kwani toka kocha huyo akiwa Chelsea kama unakumbuka aliuponda usajili wa Shaw kwenda Manchester United.

Wengi waliamini kauli za Jose Mourinho huenda zikamkera Luke Shaw, huku wengi wakidhani labda safari ya Shaw kwenda Man City ndio itakuwa imeiva, lakini Shaw ameibuka na kumjibj Mourinho kivingine.

Shaw ameibuka na kuvunja ukimya kuhusu kauli za kocha Jose Mourinho, Shaw amesisitiza kwamba atapambana kwa kuwa kocha huyo amemtaka apiganie namba baasi yeye yuko tayari kupambana.

“Nataka kucheza kwa ajili ya kocha wangu lakini vile vile nipambane kuirejesha timu hii juua” alisema Shaw mchezaji wa zamani wa Southampton, United bado wanaonekana kuteswa na nafasi ya beki wa kushoto kwani toka Shaw arudi kutoka majeraha aliyoyapataga ameahindwa kurudi katika kiwango chake.

Kuhusu kuhusishwa na kuondoka katika klabu hiyo, Shaw amekanusha taarifa hizo na kusisitiza anaipenda Manchester United na ataendelea kubaki katika timu hiyo hadi mengineyo yatakapotokea.

“Naipenda timu hii kwanj mashabiki wake wamekuwa bora sana kwetu katika siku za hivi karibuni, napambana sana kurudi katika ubora wangu ili kila mtu aamini siko hapa kwa bahati mbaya” alisema Shaw.

Shaw amesema kwamba katika kipindi hiki anafanya sana mazoezi kuliko wakati wowote ule ili kumthibitishia Mourinho na wote wasiomuamini kuwa wamekosea, Shaw amepoteza namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Manchester United na amepanga kuipigania namba yake kwa nguvu zote.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here