Home Kimataifa Russell Westbrook Aweka Rekodi Ya Kipekee NBA.

Russell Westbrook Aweka Rekodi Ya Kipekee NBA.

2303
0
SHARE

Mara ya mwisho ilikuwa msimu wa 1961-1962 ambapo mchezaji Oscar Robertson maarufu kama Big O alimaliza msimu wa NBA akiwa na wastani wa Triple Double Yaani kwa wasioelewa hiki kitu ni kuwa kupata walau alama kumi kwenye sehemu tatu tofauti za takwimu. .

Russell Westbrook amekuwa na msimu bora kabisa kwa mchezaji yoyote wa NBA kwani alfajiri ya leo amefanikiwa kufikia rekodi ya Big O kwa kupata triple double yake ya 41 baada ya kufunga pointi 12 kutoa assists 13 na kudaka rebound 13 katika mchezo walioshinda kwa pointi 110-79 dhidi ya Milwaukee Bucks.

Kumekuwa na maswali mengi juu ya mchezaji gani anastahili kushinda Tuzo ha MVP msimu huu. James Harden ameifanya Houston Rockets kuwa hatari sana tangu ahamishiwe eneo la Point Guard na kocha wao mpya Mike D’Anton na wamekuwa na msimu bora kupita kiasi. Lakini anachofanya Russell Westbrook kinaonekana kuwa cha kipekee zaidi na Inawezekana kabisa akashinda tuzo hii. .

Ingawa kwa misimu iliyopita na historia ya NBA timu nje ya nafasi 5 za juu huwa ni nadra sana kushinda MVP. Ila kwa Russell inaweza kuwa tofauti kutokana na rekodi anayoweka.

MVP MVP MVP MVP MVP ndio kelele zilizokuwa zinaongoza uwanjani wakati klabu ya OKC ikipata ushindi mzuri dhidi ya BUCKS ambao hawakuonekana kuwa wale waliozoeleka hasa katika nusu ya pili ya mzunguko wa NBA msimu huu. Mashabiki wa OKC Thunder wakimuimbia Russell Westbrook muda wote na sura yake ilionyesha kukubaliana na hilo.

HIGHLIGHTS

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here