Home Kimataifa Rais Wa Uefa Azilaumu Ligi Kubwa Kwa Ulaghai Dhidi Ya Uefa.

Rais Wa Uefa Azilaumu Ligi Kubwa Kwa Ulaghai Dhidi Ya Uefa.

4677
0
SHARE

Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin amezishutumu ligi kubwa za Ulaya kwa kujaribu kushirikiana kulilaghai shirikisho hilo kwenye mambo mbalimbali hasa ushiriki wa vilabu vyao kwenye mashindano ya Ulaya.

Chama kinachowakilisha ligi za Ulaya ambacho kina wanachama kutoka katika nchi 25 maarufu kama (EPFL), kimekua kikienda kinyume na kuipinga UEFA tangu kuachwa kushirikishwa kwenye mabadiliko ya maingizo kwenye klabu bingwa Ulaya na mgawanyo wa fedha za washindi.

Makubaliano yaliyokuwepo kati ya EPFL na UEFA juu ya kuepuka ligi kuingiliana yalimaliza muda wake mwezi uliopita, na EPFL wakasema ligi zake kwa sasa zitakuwa huru kuweka mechi katika muda unaofanana na ule wa klabu bingwa Ulaya na mechi za Europa League.

“Hatuwezi kufikiria na kuingia mtego wa ulaghai kutoka kwa wale wanaoamini kuwa wanaweza kuzizunguka na kuzitumia ligi ndogo katika kutaka kuweka adhima yao ndani ya mashirikisho kadhaa kwa sababu tu wanaamini wanaweza kufanya hivyo kutokana na nguvu wanayopata kutokana na mapato ambayo ligi za ndani za nchi zao zinaingiza,” Ceferin alisema kwenye mkutano wa UEFA.

Ceferin pia alisema UEFA wanajiandaa kuchunguza juu ya ukatili kijinsia kwenye soka hasa kwa vijana baada ya shutuma kadhaa zilizotoka kwenye mashirikisho kadhaa hasa huko Uingereza kwa miezi ya karibuni.

Rais wa FIFA  Gianni Infantino alihudhuria mkutano huo na kusema kuwa  uchaguzi uliomweka Ceferin madarakani mwaka jana ulimaliza uadui uliokuwepo katia ya UEFA na FIFA.

“Huu ni upinzani wa kipuuzi kati ya UEFA na FIFA ambao haupo tena na ambao hautakiwi kuwepo,” Infantino alisema kabla hajamkumbatia Ceferin.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here