Home Kitaifa Yanga imewaruhusu wachezaji wanaotaka ‘kusepa’

Yanga imewaruhusu wachezaji wanaotaka ‘kusepa’

16305
0
SHARE

Na Zainabu Rajabu

MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Yanga SC inayoongoza ligi mpaka sasa kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya mahasimu wao Simba huku kila timu ikibakiwa na mechi tano kumalizika msimu huu.

Timu ya Yanga Jumamosi ya wiki hii itacheza mechi ya Play-off ya kombe la shirikisho Afrika dhidi ya MC Alger katika uwanja wa Taifa na watarudiana wiki moja baadae huko Algeria.

Kuelekea mwisho wa msimu Uongozi wa Yanga umetoa ruhusa kwa mchezaji yoyote kuondoka Yanga iwapo tu atafuata taratibu, Katibu wa Yanga Boniface Mkwasa alisema.

“Kama kuna Mchezaji anataka kuondoka basi awe muungwana, atueleze mapema na taratibu zifuatwe, Pia kama kutakuwa na mchezaji ambaye Mwalimu anona hamuhitaji sisi tutafuata taratibu na kumueleza mapema kabisa.”

Wakati akiyasema hayo Mkwasa kuna hatari timu ya Yanga ikawakosa wachezaji wengi muhimu ambao mikataba yao inaelekea kuisha ndani ya Yanga, Wazimbambwe wawili Donald Ngoma na Thabani Kamusoko mwisho wa msimu mikataba yao inaisha na uongozi wa Yanga haijaweka bayana kuhusu kuwaongezea mikataba mipya.

Pia mabeki wa kati wazawa Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ mikataba yao inafikia tamati mwisho wa msimu, hivyohivyo kwa mshambuliaji Anthony Mateo na beki wa kimataifa wa Togo Vicent Bossue.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here