Home Kitaifa Dakika 10 za maajabu ya Serengeti Boys vs Ghana

Dakika 10 za maajabu ya Serengeti Boys vs Ghana

22216
0
SHARE

Dakika 10 za muda wa nyingeza, zilitosha kwa Serengeti Boys kutoka nyuma kwa magoli 2-0 na kusawazisha magoli yote kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya vijana wa U17 ya Ghana.

Kwa dakika zote 90 za mchezo Serengeti Boys ilikua nyuma kwa magoli 2-0 dhidi ya Ghana magoli yaliyofungwa na Sulley Ibrahim dakika ya 21 kipindi cha kwanza na Arko Mensah dakika 75 kipindi cha pili.

Kutokana na wachezaji wengi wa Ghana kuanguka mara kwa mara ndani ya uwanja na kulazimika kupatiwa huduma ya kwanza na madaktari wao, dakika 10 ziliongezwa kama fidia ya muda uliopotea ndani ya dakima 90.

Dakika hizo 10 unaweza kuziita za maajabu kwa sababu vijana wa Serengeti walikuja juu na kulisakama goli la Ghana kwa muda wote kutafuta namna ya kuwafurahisha watanzania.

Msako mkali uliofanywa na Serengeti Boys kwenye goli la Ghana ulizaa ‘tuta’ lililotokana na beki wa Ghana kuushika mpira ndani ya eneo la hatari wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa hatari golini kwake.

Assad Juma akakwamisha kambani mkwaju wa penati na kuiandikia bao la kwanza Setengeti Boys ambalo liliwapa morali ya kutafuta bao la kusawazisha.

Wakati watu wengi wakiamini mwamuzi atamaliza mchezo huku matokeo yakiwa Tanzania 1-2 Ghana, ndipo vijana walipofanya maajabu kwa kusawazisha goli dakika ya mwsho kabisa.

Muhsin Makame ndiye aliyerudisha furaha iliyopotea kwa watanzania akipasia kambani kwa ulaini krosi iliyompta golikipa wa Ghana na kufanya matokeo kusomeka 2-2.

Mechi hizi za kirafiki ni mfululizo wa maandalizi kwa Serengeti Boys kabla ya kwenda kwenye michuano ya Afrika (AFCON) kwa vijana wenye umri wa miaka chini ya 17 inayotarajiwa kuanza mwenzi Mei huko Gabon.

Taarifa zaidi inakujia….

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here