Home Kimataifa Wachezaji maarufu walioko katika hatihati kulikosa kombe la dunia 2018.

Wachezaji maarufu walioko katika hatihati kulikosa kombe la dunia 2018.

9474
0
SHARE

Gareth Bale. Ni muujiza tu ndio wa kuwavusha Wales kwenda Urusi mwaka 2018, hadi sasa hawajafungwa lakini nafasi yao kufudhu kwa kombe la dunia ni ndogo. Katika michezo yao mitano iliyopita wamepata suluhu 4 na kufungwa mchezo mmoja na mechi inayofuata dhidi ya Serbia watamkosa Gareth Bale.

Riyad Mahrez. Hadi sasa katika kundi lao ni timu inayoburuza mkia, uhakika wa wao kufudhu kwa ajili ya kombe la dunia ni mdogo sana, mchezaji huyo bora wa Afrika naye anaweza kuyaangalia mashindano hayo katika video tu kama mashabiki wengine.

Sadio Mane. Mane kama ilivyo kwa Mahrez anaweza kukosa fainali zijazo za kombe la dunia, hii ni bahati mbaya sana kwake akiwa na timu ya taifa kwani hata fainali za AFCON walikosa kombe na yeye ndiye aliyekosa penati. Baada ya kipigo toka kwa Bafanabafana wako nafasi ya tatu huku wakiwa na mechi ngumu dhidi ya Burkina Fasso.

Alexis Sanchez. Kipigo kutoka kwa Argentina kimewapeleka Chile hadi nafasi ya tano kwenye group lao, kombe la dunia lililopita walikuwa gumzo lakini sasa itawapasa kuchukua pointi nyingi katika mechi zijazo huku mchezo wao wa mwisho wakicheza dhidi ya Brazil ambao toka wapate kocha mpya hawajapoteza mchezo hata mmoja.

Artulo Vidal. Kama ilivyo kwa Sanchez, Vidala ni mchezaji mwingine ambaye katika fainali zilizopita za kombe la dunia alikuwa gumzo akiwa na timu yake ya Chile lakini safari hii mambo sii mambo na imebaki michezo minne tu kuamua hatma yao juu ya mashindano ya kombe la dunia mwaka 2018.

Arjen Robben. Tayari kocha wa Uholanzi ambaye ni baba mzazi wa Dalley Blind ameshatimuliwa kutokana na matokeo mabovu yanayoiandama timu hiyo. Kipigo cha bao 2 kwa 0 kutoka kwa Bulgaria kimezifanya ndoto za Uholanzi kwenda Urusi 2018 kuanza kufifia taratibu na hivyo Robben nae anaweza kuitizama michuano hiyo kama mshabiki tu.

Pierre Aubemayang. Moja kati ya wachezaji bora Africa na ligi ya Ujerumani ni Aubemayang, lakini nao nafasi yao kufudhu ni ndogo kwani vinara Ivory Coast nao wanaihitaji nafasi hiyo huku wakiwa wanaongoza kundi lao.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here