Home Ligi EPL Thierry Henry Aitamani Kazi Ya Ukocha Arsenal.

Thierry Henry Aitamani Kazi Ya Ukocha Arsenal.

4854
0
SHARE

Jina la Thierry Henry ni maarufu kwenye masikio ya mashabiki wa Arsenal kutokana na nguli huyo kufanya makubwa kwenye historia ya klabu hiyo akiwa kama mchezaji huku pia ikiwa mfungaji bora kuwahi kuvaa jezi za klabu hiyo. Lakini sio maarufu kwa upande wa ufundi kwa maana ya kazi ya Ukocha.

Taarifa kadhaa kwa siku za karibuni zilimhusisha mchezaji huyo na kutaka kupewa kazi ya ukocha wa Arsenal achukue nafasi ya Wenger. Na katika kutia sukari kwenye chai inayochemka Thierry Henry amegoma kuondoa uwezekano wa yeye kuchukua nafasi ya Wenger kama kocha wa klabu ya Arsenal .

Akiwa ni kocha msaidizi kwa sasa kwenye nchi ya Ubelgiji chini ya kocha mkuu Roberto Martinez, Henry amekiri kuwa bado yupo katika mwendelezo wa kujifunza maisha ya ukocha.

Wenger amekuwa katika mgandamizo mkubwa kipindi hiki kutokana na matokeo ambayo klabu ya Arsenal imeendelea kuyapata na Henry ambaye pia ni mchambuzi wa Sky Sports amekiri kuwa angependa kuja kuwa kocha wa klabu hiyo mbeleni.

“Hiyo hainitegemei mimi, kuna vitu inabidi viheshimiwe, ni klabu ninayoipenda kwa moyo wangu wote lakini sina mbawa kamili,” Henry alisema.

“Jina langu limekuwa likinukuliwa kumrithi Wenger, nimekuwa nikisikia hilo. Lakini ni ngumu mimi kuzungumzia hilo kwa sababu naheshimu yote ambayo kocha huyo kaifanyia klabu hiyo.

“Je nipo tayari? Sifahamu na hakuna anayefahamu, lakini pia natakiwa kujifunza zaidi juu ya kazi yangu.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here