Home Kimataifa Kutoka Chelsea hadi kusikojulikana, yuko wapi Adam Nditi?

Kutoka Chelsea hadi kusikojulikana, yuko wapi Adam Nditi?

25012
0
SHARE

Maswali yamekuwa mengi kuhusian na alipo kwa sasa Mtanzania Adam Nditi ambaye alikuwa akiichezea Chelsea, miongoni mwa watu waiohoji alipo Nditi ni mkali wa Bongofleva Juma Jux na mchezaji wa klabu ya Genk Mbwana Samatta.

ShaffihDauda.com bado inaendelea kumtafuta Nditi mwenyewe ajibu swali hili lakini si vibaya tukawapa rekodi za usajili wake tangu aende Uingereza hadi alipoonekana mara ya mwisho akicheza mpira.

Kwa mara ya kwanza mwaka 2008 ma-scout wa Chelsea walimuona Nditi akicheza mpira huko Basingstoke, walivutiwa na uchezaji wake ndipo walipomchukua na kumpeleka Chelsea akichezea timu ya vijana kama beki wa kushoto wa timu hiyo.

Mwaka 2011 alipata nafasi ya kuichezea Academy ya Chelsea katika mechi dhidi ya Tottenham, lakini mwaka huohuo alipata bahati kuifungia Academy hiyo bao dhidi ya Academy ya Norwich, na akawa sehemu ya ushindi wa kombe la FA kwa timu yao ya vijana mwaka 2012.

Majeruhi yalianza kumuandama Nditi kuanzia mwaka 2013 lakini baada ya kurudi aliisaidia Chelsea kuchukua ubingwa wa wachezaji chini ya miaka 21. Baada ya majeruhi ya muda mrefu Chelsea waliamua kuachana nae mwaka 2013, na hii kumfanya nusu msimu wa mwaka 2014/2015 kutokuwa na timu.

Baadae alijiunga na klabu ya Fletwood Town ambayo hakumaliza hata mwaka mmoja akahamia Farnborough Fc kama mchezaji huru.

Farborough nako hakudumu kwani baada ya miezi kadhaa tu alihamia bure katika klabu ya Guildford City ambako ndiko alionekana mara ya mwisho, japo nako sasa haonekani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here