Home Kitaifa Thamani halisi ya kiatu anachovaa Mbwana Samatta

Thamani halisi ya kiatu anachovaa Mbwana Samatta

33436
0
SHARE

Na Zainabu Rajabu

TUMEKUWA tukiona kwa wenzetu barani Ulaya kwa wachezaji wenyewe majina makubwa kama Cristiano Ronaldo, Lionel Messi wakivaa viatu vya mpira venye thamani ya juu zaidi duniani, tukiangalia kwa hapa Tanzania tunae mshambuliaji wa kimataifa Mbwana Ally Samatta ambae ana vaa kiatu chenye gharama ya dola 800 za Marekani zaidi ya Tsh. 1,760,000 (milioni moja laki saba na elfu sitini).

Mshambuliaji huyo anasakata kambumbu katika klabu ya KRC Genk ya Ubegiji amekuwa na msimu mzuri katika ligi kuu ya nchi hiyo huku akiisaidia timu yake kufuzu katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Europa League.

Shaffihdauda.co.tz. ilipiga stori na Mbwana Samatta ambae kwa sasa yupo nchi Tanzania katika kuitumikia timu ya Taifa (Taifa Stars) katika mechi mbili za kimataifa zinazowakabili alisema, unapokuwa mchezaji mkubwa na unatazamwa na kila mtu ni lazima uwe wa tofauti katika maisha ili uwe mfano wa kuigwa kwa hawa chipukizi wanaochipukia kwasasa.

“Siyo vibaya mimi kuvaa viatu vya gharama vya kuchezea mpira kwasababu ninaipenda kazi yangu na ndiyo maana siangali nimenunua kwa bei gani,” alisema Mbwana huku akicheka.

Aidha mchezaji huyo wa zamani wa Simba alisema wachezaji wa kitanzania wana vipaji vya hali ya juu ambavyo havipatikani kwa urahisi sehemu nyingine, lakini mababu zetu hawakuweka njia nzuri katika kuvitangaza vipaji hivyo ambavyo tunavyo kwenye hii nchi yetu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here