Home Kimataifa Yasemavyo magazeti leo barani Ulaya.

Yasemavyo magazeti leo barani Ulaya.

6268
0
SHARE

The Independent. Gazeti la Independent lenyewe kimeibuka na taarifa inayomhusisha Wayne Rooney na Everton, Independent linasema Rooney atarejea katika klabu yake ya utotoni mwishoni mwa msimu huu, tayari Rooney amaepoteza namba ya kudumu United na ni wazi anaweza ondoka.

The Sun. The Sun leo limeibuka na tetesi mbalj mbali za usajili lakini mojawapo ni mshambuliaji wa Sundetland Jermain Defoe, Defoe anadaiwa yupo katika mazungumzo ya awali na klabu ya West Ham United.
Lakini pia The Sun limesema kocha wa Liverpool Jurgen Klopp yuko mbioni kuimarisha sehemu yake ya ulinzi kwa kuleta mabeki wapya, na majina mawili ikiwemo la mlinzi wa Borussia Dortmund Mathias Ginter na mlinzi wa kushoto wa Athletico Madrid Theo Hernandez yapo kwenye orodha ya Liverpool.
The Sun hilohilo tena limeibuka na taarifa mpya kuhusiana na kiungo wa PSG ya Ufaransa Marco Verratti, Verratti anataka kuondoka PSG na sasa miamba miwili ya Hispania Real Madrid na Barcelona wanaingia vitani kutafuta saini ya kiungo huyo.
Dailly Mirror limetoa habari mbaya kwa mashabiki wa Manchester United baada ya kuandika kwamba, mlinzi wa Manchester United Phill Jonea huenda akawa nje ya uwanja kwa wiki 5 baada ya kuumizwa na mchezaji mwenzake wa Manchester Chriss Smalling wakiwa mazoezini.
Dailly Express limeeleza kwamba Real Madrid wako tayari kumuachia Isco ajiunge na Man City, lakini Madrid wako tayari kufanya hivyo endapo tu Man City nao watakuwa tayari kumruhusu Aguero ajiunge nao.
Tukimalizia na Dailly Star, katika gazeti hilo imendikwa kwamba kiungo wa Everton Ross Barkley anataka kuhamia katika timu za London,Chelsea na Tottenham ndio timu ambazo anaweza kujiunga nazo mwishoni mwa msimu

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here