Home Kimataifa Miezi 15 tu hawa wamebakiza Arsenal,watasaini mkataba mpya au wanaondoka?

Miezi 15 tu hawa wamebakiza Arsenal,watasaini mkataba mpya au wanaondoka?

5732
0
SHARE

Klabu ya Arsenal bado iko katika majanga kwani matokeo yao yamekuwa hayaridhishi,lakini pia wachezaji wengi muhimu ni kama wanataka kuondoka huku baadhi yao wakiwa wamebakiza miezi michache ya mikataba klabuni hapo,wafuatao wamebakiza miezi 15 tu na hadi sasa hawajasaini.

Alexis Sanchez. Ripoti zinasema Sanchez ameahidiwa dili jipya na nono Arsenal lakini bado anasita kusaini. Tayari kuna timu kama PSG,Juventus na timu za kutoka China zimeahidi mshahara wa zaidi ya £250,000 kwa wiki.Arsenal wanafahamika hawawezi kumpa Sanchez £280,000 kwa wiki lakini tatizo linakuja watamuuza wapi?kwani hakuna timu ambayo inanonesha nia hasa ya kumtaka hivyo wanaweza mtoa kwa bei ya hasara.

Oxlade Chamberlain. Tayari Jurgen Klopp ameshanza kufuatilia kwa karibu kuhusu suala la mkataba wake, ni mchezaji wao muhimu lakini bado naye hajasaini mkataba mpya huku miamba ya jiji la Manchester nayo ikifuatilia kwa karibu suala la mkataba wake.
Jack Wilshaire. Amekuwa na kiwango kizuri toka apelekwe Fc Bournamouth kwa mkopo, kiwango chake kimeshaanza kuzivutia timu kubwa ikiwemo United na Man City. Lakini Arsenal wana tatizo bado katika nafasi ya kiungo na hii inatia mashaka kama wakimuuza lakini pia hajapewa mkataba mpya hadi sasa.
Petr Cech.Amekuwa mhimili muhimu kwa Arsenal toka asajiliwe kutoka Chelsea, na ni miongoni mwa makipa bora katika ligi ya Uingereza. Bado Arsenal hawajampa mkataba mpya pamoja na umuhimu wake huo, na hii inatia mashaka kama ataendelea kubaki katika klabu hiyo japo akiondoka itakuwa pigo.
Santi Carzola. Majeruhi msimu huu yamemuweka nje kwa muda mrefu sana, lakini Arsenal wana mkataba naye hadi mwaka 2018. Haijafahamika kama mkataba huu utaongezwa au 2018 ndio mwisho wa Carzola kubaki katika klabu hiyo.
Per Martersacker. Mlinzi wa timu ya taifa ya Ujerumani na moja kati ya ngome za Arsenal katika ulinzi. Martersacker naye mkataba wake unaisha mwaka 2018. Lakini hadi sasa hajasainishwa mkataba mpya, umuhimu wake klabuni hapo kila mtu anaujua.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here