Home Kimataifa Habari njema kwa Chelsea na mbaya kwa Manchester United.

Habari njema kwa Chelsea na mbaya kwa Manchester United.

29313
0
SHARE

Kumekuwa na vita vya usajili juu ya wachezaji mbalimbali katika kipindi hiki ligi za Ulaya zinapoelekea ukingoni. Moja kati ya majina makubwa yanayopiganiwa sana ni kiungo mkabaji wa Monaco na timu ya taifa ya Ufaransa Tioumuae Bokoyoko.

Manchester United,Manchester City,Chelsea na PSG ni kati ya vigogo wakubwa waliokuwa wakiipigani sahihi ya Bokoyoko,lakini taarifa mpya zinadai Chelsea wanaonekana kukaribia kutimiza mbio hizo.
Taarifa zinasema Chelsea tayari wameshafanya makubaliano binafsi kati ya Bokoyoko na wao,na kinachosubiriwa sasa ni Chelsea kufanya mazungumzo na Monaco ili Bokoyoko atue Stamford Bridge kuungana na Mfaransa mweznie Ngolo Kante.
Msimu huu umekuwa mzuri sana kwa Bokoyoko katika ligi ya Ufaransa lakini pia ligi ya Champions kwani goli lake dhidi yaan City ndio liliivusha Monaco kucheza robo fainali ya mashindano hayo msimu huu.
Vivyo hivyo mwaka huu unaonekana wa mafanikio sana kwake kwani pia kwa mara ya kwanza ameitwa katika kikosi cha timu ya soka ya Ufaransa, Bakayoko ameitwa katika kikosi hicho kuchukua nafasi ya Paul Pogba aliye majeruhi.
Wakati Chelsea wakifurahia habari hii, lakini ni habari mbaya kwa mashabiki wa Manchester United, katika dirisha la usajili la mwezi wa kwanza United walikaribia kumsajili Bakayoko lakini wakaambiwa wasubiri hadi mwisho wa msimu lakini sasa wanaelekea kumkosa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here