Home Kimataifa Ferguson kurejea United tena kama kocha

Ferguson kurejea United tena kama kocha

27992
0
SHARE

Sir Alex Ferguson ndiyo nembo iliyoko nyuma ya mafanikio ya Manchester United, akiinoa United kuanzia mwaka 1986 hadi 2013 aliwapa karibia kila kombe kuanzia Uingereza, Ulaya na dunia nzima.

Tangu baada ya Ferguson kuondoka timu hiyo imekuwa ikiyumba huku makocha wawili waliomfuatia David Moyes na Luis Van Gaal wakishindwa kuwapa kile wanachotaka, huku kocha wao wa sasa Jose Mourinho kidoogo akianza kuwafurahisha.
Tayari mashabiki wa Manchester United dunia nzima walianza kupiga kelele wakitaka Ferguson arudi kutetea jahazi lao linaloonekana kuzama, kabla ya Mourinho kuanza kuwainua.
Lakini sasa kiu ya mashabiki wengi wa Manchester United ya kumuona Ferguson akiwa kwenye benchi la Old Traford kama kocha inaelekea kutimia, Ferguson atarudi kama kocha wa United tarehe 4 mwezi wa June.
Ferguson ambaye hadi anastaafu alishawapa United jumla ya makombe 26 atakuwepo kwenye mchezo maalum kwa ajili ya mchezo maalum  kwa ajili ya kiungo wa Manchester United Michael Carrick.
Ferguson katika mchezo huo atakuwa kocha wa wachezaji wa zamani wa Manchester United.Ferguson atakuwa kocha wa kikosi cha wachezaji wa zamani wa United ambao watacheza na timubya Carrick.
Pengine hii itawavutia sana mashabiki wa Manchester United, kwani toka Ferguson atangaze kustaafu hawajawahi tena kumuona akisimama nje ya uwanja kama kocha.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here