Home Kimataifa Wimbo mpya wa mashabiki wamkosha Jose Mourinho

Wimbo mpya wa mashabiki wamkosha Jose Mourinho

4765
0
SHARE

Toka katika nusu fainali ya kombe la EFL mashabiki wa Manchester United wameibuka na wimbo mpya, wimbo huo unaelezea ni jinsi gani wanavyofurahia jinsi kocha wao mpya anavyowafanya wacheze.

Katika wimbo huo kuna moja ya sehemu inasema “tulipoamka asubuhi hii tukaona mwanga,oohh jamani tunajisikia vizuri sana”,hio ndio sehemu ya maneno yanayosikika katika wimbo huo mpya.
Mourinho ameuzungumzia wimbo huo na kusema ni jinsi gani anavyojisikia kwa wimbo huo ambao haumtaji jina lake. Mourinho anasema anafurahia sana kuona mashabiki wanavyofurahia kuona jinsi anavyowaongoza msimu huu.
“Tofauti na klabu zingine nilizopita walikuwa wanaimba jina langu mara Mourinho, mara The Special One, mara Mreno, lakini hapa wana wimbo mpya na hauntaji mimi bali unaeleza hisia zao jinsi wanavyojisikia furaha.”
“Kushinda kombe la Uingereza kwa msimu huu ni ngumu sana kwakweli, ila kuna hizi hisia ambapo watu wana furaha na hicho ndiyo muhimu hapa,watu kuwa na furaha” alisema Mourinho ambaye msimu huu anaonekana kuwapa furaha kweli Manchester United.
Mourinho anaamini furaha anayowapa mashabiki itamfanya aendelee kukaa klabuni hapo kwa muda mrefu. Na kudokeza kuwa kama ni muda mchache ndani ya Manchester United atakaa kwa miaka mitatu zaidi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here