Home Kimataifa Manchester United waweka rekodi ya kushinda mara 600, timu yako je?

Manchester United waweka rekodi ya kushinda mara 600, timu yako je?

5718
0
SHARE

Baada ya kukaa kwa siku zaidi ya 100 wikendi iliyopita Manchester United wameondoka katika nafasi ya 6 na kuipisha Arsenal,magoli 3 kwa 1 ambayo ambayo United waliifunga Middlesbrough imewapandisha kwa nafasi moja juu na sasa wako nafasi ya 5.

Sio kupanda nafasi tu bali ushindi huo umeiwekea United rekodi mpya nchini Uingereza, United wameweka rekodi mpya kwa kuwa timu ya kwanza katika ligi ya Uingereza kwa kupata ushindi wa 600,hakuna timu yoyote Uingereza ambayo imeshafanya hivyo.
Ushindi huo ni wa 14 kwa Manchester United katika ligi ya Uingereza ila ni wa 600 toka klabu hiyo ianzishwe.Lakini Arsenal ambao walifungwa wikiendi hii wanaifuatia United kwa karibu katika jumla ya ushindi.
Pamoja na vipigo walivyopokea msimu huu lakini Arsenal wako nafasi ya pili wakiwa wameshinda michezo 517.Lakini vinara wa ligi ya Uingereza klabu ya Chelsea ambao msimu huu wameshinda mara 22 katika ligi ya Uingereza wako nafasi ya 3 wakiwa na jumla ya mechi 508 walizoshinda.
Liverpool wako nafasi ya 4 kama ilivyo katika ligi wakiwa wameshinda mara 472,
huku Tottenham wakiwa wameshinda jumla ya michezo 391,lakini Manchester City wanajitokeza nafasi ya 6 wakiwa wameshinda jumla ya michezo 321.
Lakini Manchester United wakiwa na ushindi mara 600, huwezi kuamini kuhusu timu ya Bournamouth Fc walioko pia katika ligi kuu ya Uingereza.Bournamouth wameshinda mechi 20 tu ikiwa ni mechi 580 pungufu ya United, huku Swindon Town wakiwa wameshinda mara 5 tu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here