Home Kitaifa ‘Kwa tulipofika, si haba’ – Mwambusi

‘Kwa tulipofika, si haba’ – Mwambusi

3984
0
SHARE

Na Zainabu Rajabu

PAMOJA na kushindwa kufuzu hatua inayofata ya michuano ya klabu bingwa Afrika, kocha Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema haikuwa kazi rahisi kushinda hatua hii na kwenda hatua ya makundi.

Akizungumza Shaffihdauda.co.tz. Mwambusi amesema: “Michuano ilikuwa migumu na tumejifunza mengi toka tumeanza kushiriki na mpaka sasa tunaondolewa, tumejipanga kukiboresha kikosi chetu katika msimu ujao.”

“Nimewaambia licha ya kushindwa kufuzu hatua ya nusu fainali lakini tumejifunza vingi kubwa ni suala la nidhamu ya mchezo na nidhamu ya mchezaji husika uwanjani,” alisema Kocha huyo wa zamani wa Mbeya City.

Mwambusi alisema: Tunajenga msingi mzuri wa timu kitaifa na kimataifa . Kwa mantiki hiyo tulipofikia si haba, watanzania watuelewe tumejenga Yanga mpya na ya ushindani,” alisema Mwambusi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here